COSTECH Integrated Repository

Wahusika wa kimimi katika riwaya ya Kiswahili: mifano kutoka dunia yao na nyuso za mwanamke

Show simple item record

dc.creator Ali, Haji Bakar
dc.date 2019-08-20T09:43:29Z
dc.date 2019-08-20T09:43:29Z
dc.date 2018
dc.date.accessioned 2019-12-06T12:20:29Z
dc.date.available 2019-12-06T12:20:29Z
dc.identifier Ali, H. B. (2018). Wahusika wa kimimi katika riwaya ya Kiswahili: mifano kutoka dunia yao na nyuso za mwanamke (Tasnifu shahada ya umahiri). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.
dc.identifier http://hdl.handle.net/123456789/1002
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/16416
dc.description Tasnifu (Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Utafuti huu ulilenga kuchunguza wahusika wa Kimimi katika riwaya za Said Ahmed Mohamed kwa kujikita katika miktadha ya utokeaji wa wahusika hao, namna wahusika wanavyojikengeusha na jamii; na sababu za wahusika kujikengeusha. Matumizi ya wahusika wa Kimimi hayajachunguzwa vya kutosha. Yumkini, hali hii inasababisha kutokufahamika miongoni mwa wasomaji na wahakiki wa kazi za fasihi. Kazi tulizozipigia mbizi kwa kina katika kuchunguza wahusika wa Kimimi ni riwaya ya Dunia Yao na Nyuso za Mwanamke. Utafiti ulifanyika maktabani. Maeneo yaliyotumika kukusanyia data ni Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Zanzibar. Hakuna data yoyote ya kitakwimu iliyotumika katika utafiti huu, bali tulitumia mbinu ya ufafanuzi. Uchambuzi wa data umefanyika kwa kutumia mkabala wa kisaikochanganuzi ambapo uchambuzi ulifanyika kwa mbinu ya ufafanuzi. Matokeo yanaonesha kuwa, riwaya ya Dunia Yao na Nyuso za Mwanamke zimetumia miktadha ya chimbuko la kifasihi, kisiasa, shereheni, kazini, kifamilia, mahakamani na mitaani.Pia, wahusika wamejikengeusha kwa kugomea chakula, kutojali, ukivuli, kutokata tamaa, kushiriki ngono, usasa, ulevi na uongozi bora. Sababu za wahusika kujikengeusha ni ukosefu wa ajira, utandawazi, ukombozi wa mwanamke, siasa, utamaduni, habari na mawasiliano na usomi. Utafiti uliongozwa na mkabala wa Saikochanganuzi.Mchango mpya ulioibuliwa na utafiti huu katika taaluma ya fasihi ni huu. Mosi, kuibuliwa kwa miktadha ambayo wahusika wa Kimimi wamesawiriwa katika riwaya ya Dunia Yao na Nyuso za Mwanamke. Pili, Kufafanuliwa sababu za wahusika kujikengeusha na jamii. Tatu, kuibuliwa kwa sababu za wahusika kujikengeusha ambazo ni ukombozi, siasa, utamaduni na usomi.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Kimimi
dc.subject Nyuso
dc.subject Mwanamke
dc.subject Dunia
dc.subject Fasihi
dc.subject Tamaa
dc.subject Usasa
dc.subject Ulevi
dc.subject Ajira
dc.subject Ukombozi
dc.subject Maadili
dc.title Wahusika wa kimimi katika riwaya ya Kiswahili: mifano kutoka dunia yao na nyuso za mwanamke
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account