COSTECH Integrated Repository

Taswira katika ushairi wa Mwinyihatibu: Kutoka malenga wa Mrima na malenga wa Mrima nimerudi

Show simple item record

dc.creator Taufiq, Bisibo
dc.date 2019-08-19T07:25:46Z
dc.date 2019-08-19T07:25:46Z
dc.date 2016
dc.date.accessioned 2019-12-06T12:20:30Z
dc.date.available 2019-12-06T12:20:30Z
dc.identifier Taufiq, B. (2016). Taswira katika ushairi wa Mwinyihatibu: Kutoka malenga wa Mrima na malenga wa Mrima nimerudi (Tasnifu shahada ya uzamili). Chuo Kikuu cha Dododma, Dodoma.
dc.identifier http://hdl.handle.net/123456789/842
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/16444
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Utafiti huu umechunguza Taswira katika Ushairi wa Mwinyihatibu: kutoka Malenga wa Mrima na Malenga wa Mrima Nimerudi. Chimbuko la tatizo la utafiti huu limetokana na kutoeleweka kwa ujenzi wa taswira kwa wasomaji na wasikilizaji wa ushairi. Kwa hivyo, utafiti huu umechunguza taswira katika diwani teule za Mwinyihatibu jinsi zinavyoundwa na makundi yake. Utafiti huu umeongozwa na malengo matatu, ambayo kwanza ni kuchunguza miktadha inayopelekea ubunifu wa taswira katika diwani za mshairi teule. Pili, kubainisha aina za taswira na maana zake na tatu ni kuchunguza athari chanya na hasi za taswira hizo kwa jamii. Aidha, mapitio ya utafiti huu yaligawanyika katika makundi matatu. Kwanza, mapitio yanayohusiana na dhana ya taswira, pili, ni mapitio yanayohusiana na mgawanyo wa taswira na tatu ni yale yanayohusiana na taswira katika ushairi.Nadharia iliyotumika ni umuundoleo. Utafiti huu umetumia mbinu ya kudurusu maandiko maktabani pamoja na usaili. Maeneo yaliyotumika kukusanya data ni Dodoma, Dar es Salaam na Tanga. Pia, mbinu ya ufafanuziimetumika katika kutoa matokeo ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu, yanaonesha kuwa diwani za mshairi teule zimesheheni taswira za kizuolojia, kibotania, kijiolojia, kiteolojia, kiastronomia na zile za vitu vya kawaida. Aidha, athari chanya na hasi ya matumizi ya taswira kwa wasomaji na wasikilizaji zimebainishwa.Sampuli zilizotumika katika utafiti huu zimegawanywa katika makundi manne ambayo ni diwani teule za mshairi Mwinyihatibu. Wanataaluma waliozisoma, kuzihakiki na kuzifanyia utafiti kazi za Mwinyihatibu.Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na Dar es salaam wa shahada za awali wanaosoma masomo ya Fasihi ya Kiswahili.Wenyeji wa Tanga mjini na kijijini kwao Tongoni wanaofahamu maisha ya mshairi mteule walihojiwa.Mwisho wa utafiti huu,umebainisha muhtasari wa utafiti, matokeo ya utafiti, changamoto za utafiti, mapendekezo ya utafiti na michango mipya ya kitaaluma iliyojitokeza katika utafitihuu vyote vimeoneshwa.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Ushairi
dc.subject Taswira
dc.subject Utafiti
dc.subject Ushairi
dc.subject Chimbuko
dc.subject Mshairi
dc.subject Kijiolojia,
dc.title Taswira katika ushairi wa Mwinyihatibu: Kutoka malenga wa Mrima na malenga wa Mrima nimerudi
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account