COSTECH Integrated Repository

Muundo wa Lugha Katika Mashairi ya Watungaji Wateule wa Zanzibar

Show simple item record

dc.creator HAMAD, Asha Muhene
dc.date 2020-06-08T06:45:30Z
dc.date 2020-06-08T06:45:30Z
dc.date 2017-11
dc.date.accessioned 2020-08-12T14:33:04Z
dc.date.available 2020-08-12T14:33:04Z
dc.identifier http://repository:8080/xmlui/handle/123456789/106
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/38107
dc.description Available in print form, Tunguu Reference Library
dc.description Utafiti huu unahusu “Muundo wa Lugha katika Mashairi ya Watungaji Wateule wa Zanzibar”. Diwani nne za watungaji wawili wa Zanzibar zilichambuliwa. Diwani hizo ni Kina cha Maisha ya Mohamed (1984) na Jicho la Ndani ya Mohamed (2002). Diwani nyengine ni Andamo iliyoandikwa na Ghassani (2016a) na Siwachi Kusema pia ya Ghassani (2016b). Utafiti huu ulifanywa katika Wilaya ya Magharibi A, Magharibi B na Wilaya ya Kusini, Unguja, Zanzibar. Data za msingi zilipatikana kwa njia ya maktaba, usaili kwa wahakiki wa fasihi na hojaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Zanzibar. Njia ya maktaba iliwezesha kupata data nyingi za msingi zilizotimiza malengo ya utafiti. Malengo hayo ni kuchunguza vijenzi vya lugha katika ngazi ya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki, vilivyoyajenga mashairi ya watungaji wateule wa Zanzibar kimaana na kiujumi. Aidha, utafiti ulichunguza ukiushi wa kanuni za kisarufi katika mashairi hayo na jinsi vijenzi vya lugha vilivyopambanua mtindo. Nadharia ya Umuundo na Umuundoleo zilitumika katika uchambuzi wa data. Utafiti umeonesha kuwa watunzi wote wamevitumia vijenzi vya lugha katika ngazi ya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki kuyajenga mashairi yao. Watunzi wote wamevitumia vijenzi vya lugha kwa kuzingatia kanuni za lugha kwa usahihi kulingana na muktadha, mazingira na wakati. Aidha, wamevisarifu vijengo vya lugha kuimarisha sanaa zao kiujumi na kimaana kwa kuzingatia sifa za lugha ya kishairi inayoendana na mkwepo wa sarufi. Hali hiyo imedhihirisha kuwa upo ufungamanifu kati ya vijenzi vya kimuundo na ushairi, kwa kuwa vijenzi hivyo ndivyo vilivyotumika kuyajenga mashairi ya watungaji wateule wa Zanzibar.
dc.format application/pdf
dc.language other
dc.publisher The State University of Zanzibar (SUZA)
dc.subject 1. Vijenzi vya lugha- Mashairi 2. Mashairi - Zanzibar i. Title
dc.title Muundo wa Lugha Katika Mashairi ya Watungaji Wateule wa Zanzibar
dc.type Thesis


Files in this item

Files Size Format View

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account