Available in print form, Tunguu Reference Library
Kazi hii inahusu Uchambuzi wa Nyimbo za Uganga wa Pepo Zanzibar: Mtindo n Dhima zake (Mifano kutoka jamii ya Watumbatu). Katika tasnifu hii nyimbo za uganga wa pepo wa aina tatu zilikusanywa na kuchambuiwa. Nyimbo hizo ni za uganga wa pepo wa maruhani, rumbamba na puuwo. Utafiti ulifanywa katika vijiji vya Chaani Masingini, Mkwajuni, Kibeni na Tumbatu Kichangani. Katika maeneo hayo uganga uliohusika unafanywa sana na wakaazi wake. Lengo kuu la utafiti huu lilikua kufanya uchambuzi wa mtindo na dhima za nyimbo za uganga wa pepo.
Waganga, wari, na wataalamu wa fasihi ya Kiswahili walitumiwa kutoa taarifa juu ya uanga na nyimbo zake. Watoa taarifa hao walikua wazee na vijana- wanawake na wanaume. Katika uchambuzi, tulichambua vipengele vya mtindo wa nyimbo za uganga w pepo kwa kutumia njia ya maelezo. Tulitumia mbinu ya umakinifu (ushuhudiaji) wamahojiano au usaili katika kukusanya data za utafiti. Aidha katika uchambuzi wa nyimbo za uganga wa pepo tulitumia nadharia za umuundo, dhima na kazi.Nadharia hizi zilisaidia sna katika kufanikisha uchambuzi wa nyimbo hizo.
Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa nyimbo za ugnga wa pepo zemetungwa na kuimbwa kwa kutumia vipengele vya matumizi ya maneni, takriri neon, anaphora, epifora, tasai, taksila, tasako, tempo na sauti, usambamba, tanakuzi, mtindo wa nyimbo huru, mtindo wa kutumia mshoro mmoja na mtindo wa kupokezana katika uimbaji. Kila mtindo ulikua na dhima yake kama vile kusisitiza jambo, kuvutia hadhir, kudokeza asili yawimbo na kuufanya wimbo kuimbika na kuhifadhika kwa urahisi. Aidha tulibaini kuwa nyimbo hizo zilikuwa na dhima mbalimbali kama vile kubembeleza, kujuvya, kuchombeza na kuhamasisha.