Available in print form, Tunguu Reference Library
Utafiti huu unahusu matumizi ya kipashio ‘ni’ katika Kitumbatu. Utafiti umefanywa katika Wilaya ya Kaskazini A, katika Wilaya ndogo ya Tumbatu, Unguja, Zanzibar. Data za msingi zimepatikana kwa njia ya usaili, uchunguzi makini na masimulizi kutoka kwa wanafunzi na walimu wa Skuli za Sekondari za Tumbatu pamoja na wazee kutoka katika shehia ya Jongowe na Gomani. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha aina za maneno ambazo huchukua kipashio ‘ni’ katika Kitumbatu. Kufafanua mazingira ya utokeaji wa kipashio ‘ni’ katika maneno ya Kitumbatu. Kujadili dhima ya kipashio ‘ni’ katika maneno ya Kitumbatu. Nadharia ya Umuundo imetumika katika utafiti huu. Utafiti umeonesha kuwa kipashio ‘ni’ katika Kitumbatu kina matumizi mbalimbali kwa watumiaji wa lahaja hiyo yaani Watumbatu. Miongoni mwa matumizi hayo ni kipashio ‘ni’ kama kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja mtenda na mtendwa, kielezi cha mahali, kiwakilisha cha tukio, mzizi wa neno wenye hadhi ya swali na kitenzi kishirikishi. Utafiti huu ni muhuimu kwa sababu unawasaidia walimu, wanafunzi na watafiti wa somo la lughawiya katika kupata marejeo.