COSTECH Integrated Repository

Tathmini ya Mbinu za Kufundishia Stadi ya Kuandika Kiswahili kama Lugha ya Kigeni Zanziba:

Show simple item record

dc.creator KAHINDI, Saada Said
dc.date 2020-05-18T08:08:39Z
dc.date 2020-05-18T08:08:39Z
dc.date 2019-12
dc.date.accessioned 2020-08-12T14:55:54Z
dc.date.available 2020-08-12T14:55:54Z
dc.identifier Saada Said Kahindi
dc.identifier http://repository:8080/xmlui/handle/123456789/93
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/38117
dc.description Available in print form, Tunguu Reference Library
dc.description Utafiti huu ulifanyika kisiwani Unguja, katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, taasisi mbili zilichanguliwa kushiriki katika utafiti huu. Moja ya taasisi hiyo ni ya kiserikali na nyengine ni taasisi binafsi. Lengo kuu la utafiti huu ni kutathmini mbinu wanazozitumia walimu katika kufundisha stadi ya kuandika Kiswahili kama lugha ya kigeni kwa kuzingatia kipengele cha utungaji. Watafitiwa katika utafiti huu walikuwa ni walimu wanaofundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Taasisi ya Kiswahili na Kiswahili na Utamaduni (KIU) ambazo kieneo zote zinapatikana Zanzibar. Mbinu mbalimbali za kukusanyia data ambazo ni usaili, dodoso na ushuhudiaji zilitumika katika kupata data zenye uhakika na zenye kuaminika. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa, ni kweli kuna mbinu ambazo walimu wanazitumia katika kufundishia stadi ya kuandika. Walimu wanatumia mbinu kama vile mbinu ya picha, hadithi, ziara za kimasomo, barua na mbinu jumuishi/mseto katika kufundisha stadi ya kuandika Kiswahili kama lugha ya kigeni hasa katika kipengele cha utungaji. Kutokana na matokeo na mapendekezo ya utafiti pamoja na watafitiwa imegundulika kwamba walimu hawana mafunzo ya kutosha juu ya stadi za lugha, pia muamko katika ufundishaji wa stadi ya kuandika ni mdogo sana ingawa mbinu za kufundishia zipo wazi bado kunahitajika ushajihishaji wa hali ya juu kwa wanafunzi. Katika utafiti huu, mtafiti alipendekeza taasisi zenye dhima ya kufundisha Kiswahilikama lugha ya kigeni Zanzibar, zijaribu kuandaa warsha za mafunzo ya mbinu za kufundishia stadi za lugha hasa stadi ya kuandika.Hali hii itasaidia walimu katika kuboresha ufundishaji wao wa stadi hii na stadi nyengine za lugha. Mwisho kabisa, mtafiti alishauri tafiti nyengine zifanyike ili kuziba pengo lililoachwa na watafiti wengine, na watafiti wajikite zaidi katika stadi za lugha hasa Kiswahili kama lugha ya kigeni.
dc.format application/pdf
dc.language other
dc.publisher The State University of Zanzibar (SUZA)
dc.subject Mbinu za ufundishaji kiswahili kwa wageni
dc.subject stadi ya kuandika kiswahili kama Lugha ya kigeni
dc.title Tathmini ya Mbinu za Kufundishia Stadi ya Kuandika Kiswahili kama Lugha ya Kigeni Zanziba:
dc.title Kipengele cha Utungaji
dc.type Thesis


Files in this item

Files Size Format View

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account