COSTECH Integrated Repository

Vitendoneni Katika Hotuba za Kampeni za Uchaguzi za Mwaka 2015, na Athari zake kwa Wanajamii wa Zanzibar

Show simple item record

dc.creator HAJI, Mahmoud Yussuf
dc.date 2020-06-05T07:36:21Z
dc.date 2020-06-05T07:36:21Z
dc.date 2018-12
dc.date.accessioned 2022-10-21T07:16:44Z
dc.date.available 2022-10-21T07:16:44Z
dc.identifier http://repository:8080/xmlui/handle/123456789/101
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/85094
dc.description Available in print form, Tunguu Reference Library
dc.description Utafiti huu Umechunguza Vitendoneni Katika Hotuba za Kampeni za Uchaguzi za Mwaka, 2015 na Athari Zake kwa Wanajamii wa Zanzibar. Huu ni utafiti wa uwandani uliojumuisha matumizi ya mbinu shirikishi, usaili na maktabani katika kukusanya data na hatimaye data zimechambuliwa kwa njia ya kimaelezo na kitakwimu. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa. 1) Kubainisha vitendoneni vinavyojitokeza katika hotuba za kampeni za uchaguzi za Zanzibar. 2) Kuchambua nia na nguvu za tamko kwa wazungumzaji kwenda kwa hadhira wanaosikiliza hotuba za kampeni za uchaguzi za Zanzibar. 3) Kuchambua athari hasi na chanya za vitendoneni kwa wanajamii wanaosikiliza hotuba za kampeni za uchaguzi za Zanzibar. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Kitendoneni iliyoasisiwa na Austin, (1962) pamoja na Nadharia ya Umaanishi iliyoasisiwa na Grice (1975). Jumla ya vitendoneni athari vilikuwa, 120 ambapo vitendoneni vyenye mwelekeo chanya ni 90 ikiwa sawa na 75% na vitendoneni vyenye mwelekeo hasi ni 30 ikiwa sawa na 25%. Imegundulika kuwa vitendoneni vilivyojitokeza katika hotuba za kampeni za uchaguzi vina athari chanya na athari hasi kwa hadhira. Utafiti huu umeonesha kuwa, baadhi ya wazungumzaji wanatumia vitendoneni vinavyokiuka utaratibu wa mazungumzo na baadhi yake wanatumia vitendoneni vinavyozingatia utaratibu wa mazungumzo. Aidha imebainika kuwa yapo matamko ndani yake zimo kauli zisizokubalika kutamkwa na wazungumzaji mbele ya hadhira. Vile vile yapo matamko ambayo ndani yake zimo kauli zinazokubalika kutamkwa na wazungumzaji mbele ya hadhira. Mbali na hayo, wamekuwepo wazungumzaji wanaozingatia muktadha wa mazungumzo mbele ya hadhira na wanaokiuka muktadha wa mazungumzo mbele ya hadhira kiasi ya kuchangia mawazo yenye mtazamo hasi na mawazo yenye mtazamo chanya kwa hadhira. Pia imebainika kuwa yapo matamko ya hotuba ambayo ndani yake yanatumia kanuni za ushirikiano pamoja na kanuni za unyenyekevu
dc.format application/pdf
dc.language other
dc.publisher The State University of Zanzibar (SUZA)
dc.subject 1. vitendoneni vinavyojitokeza katika hotuba za kampeni za uchaguzi za Zanzibar.
dc.subject 2. Athari hasi na chanya kwa wanajamii wanaosikiliza hotuba za kampeni za uchaguzi za Zanzibar
dc.title Vitendoneni Katika Hotuba za Kampeni za Uchaguzi za Mwaka 2015, na Athari zake kwa Wanajamii wa Zanzibar
dc.type Thesis


Files in this item

Files Size Format View

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account