COSTECH Integrated Repository

Kuchunguza Motifu za Kisasi katika Hadithi Simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja

Show simple item record

dc.creator KUTUTWA, Ramadhan Abdala
dc.date 2020-05-29T06:49:40Z
dc.date 2020-05-29T06:49:40Z
dc.date 2019-04
dc.date.accessioned 2022-10-21T07:16:44Z
dc.date.available 2022-10-21T07:16:44Z
dc.identifier http://repository:8080/xmlui/handle/123456789/96
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/85101
dc.description Available in print form, Tunguu Reference Library
dc.description Utafiti huu ulilenga kuchunguza motifu za visasi katika hadithi simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Motifu ni miegamo ambayo fanani wa kazi za fasihi huiegemea katika kuzijenga kazi zao. Visasi ni aina ya hukumu, ambayo mara nyingi, huchukuliwa na kutekelezwa pale pasipokuwa na maadili ya kikanuni. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni; kubainisha aina za motifu za kisasi zinavyojitokeza katika hadithi simulizi, kubainisha sababu za kulipizana kisasi katika hadithi simulizi, na lengo la tatu ni kuchunguza uhalisia wa visasi kwenye jamii ya mkoa wa Mjini Magharibi. Nadharia ya Uhalisia ilitumika kuchambua motifu za visasi zinazojitokeza katika hadithi simulizi na uhalisia wa visasi katika Mkoa wa Mjini Magharibi. Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni maktaba na uwandani. Data zilizokusanywa zimechambuliwa kwa kutolewa ufafanuzi wa kimaelezo na mjadala. Matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha uhalisia wa visasi ndani ya jamii ya watu wa Mkoa wa Mjini Magharibi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, kuna aina tatu za motifu za visasi ambazo ni motifu za visasi vya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa upande wa sababu za visasi, matokeo ya utafiti yamebaini kuwa kuna sababu kama vile chuki ya mali, dhuluma, wivu, bezo na husda. Aidha lengo la mwisho la utafiti huu, limebaini uhalisia wa visasi vinavyotokana na uchumi na jamii. Utafiti huu ni muhimu kwani umesaidia kuchunguza na kubainisha motifu za kisasi zilizomo katika hadithi simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibui Unguja na hivyo utawasaidia wengi miongoni mwa wasomi na wanajamii kwa ujumla.
dc.format application/pdf
dc.language other
dc.publisher The State University of Zanzibar (SUZA)
dc.subject 1. Aina za motifu za kisasi zinavyojitokeza katika hadithi simulizi
dc.subject 2. Sababu za kulipizana kisasi katika hadithi simulizi
dc.subject 3. Uhalisia wa visasi kwenye jamii ya mkoa wa Mjini Magharibi.
dc.title Kuchunguza Motifu za Kisasi katika Hadithi Simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
dc.type Thesis


Files in this item

Files Size Format View

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account