COSTECH Integrated Repository

Usasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa:

Show simple item record

dc.creator MOHAMED, Omar Salum
dc.date 2020-06-05T08:34:56Z
dc.date 2020-06-05T08:34:56Z
dc.date 2018-01
dc.date.accessioned 2022-10-21T07:16:44Z
dc.date.available 2022-10-21T07:16:44Z
dc.identifier http://repository:8080/xmlui/handle/123456789/103
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/123456789/85104
dc.description Available in print form, Tunguu Reference Library
dc.description Utafiti huu unahusu ‘Usasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa’. Mashairi ya nyimbo kadhaa wa kadhaa za taarab yamechunguzwa. Uchunguzi ulianzia na mashairi ya nyimbo za taarab halisi ambayo yametumika kama kigezo msingi katika kutambulisha usasa wa mashairi ya taarab ya sasa. Utafiti umefanyika katika wilaya tatu za Tanzania Visiwani na wilaya mbili za Tanzania Bara. Kwa upande wa visiwani ni Wilaya ya Chake Chake iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba na Wilaya ya Mjini katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Kwa Bara, ni Wilaya ya Ilala na Wilaya ya Kinondoni, Daressalaam. Malengo ya utafiti huu yalikuwa matano. La kwanza, kuainisha sifa bainifu za mashairi ya taarab halisi. La pili ni kudhihirisha mambo yaliyobadilika katika mashairi ya taarab ya sasa. La tatu ni kupambanua sababu za mabadiliko ya mashairi ya taarab ya sasa. La nne, kutathmini athari za mabadiliko ya mashairi ya taarab ya sasa. La tano ni kuchunguza namna wasanii na wapenzi wa nyimbo za taarab wanavyoyapokea mabadiliko ya fani na maudhui yaliyomo kwenye mashairi ya taarab ya sasa. Data ilipatikana kupitia mbinu ya ushiriki nafsia, mbinu ya mahojiano, mbinu ya dodoso na mbinu ya kuwa na mtafiti msaidizi. Pamoja na mbinu hizo utafiti ulitumia Nadharia ya Uamilifu, Nadharia ya Semiotiki na Unadharia Unaozama, pamoja na Mkabala wa Utafsiriji wa Vitendo na Mkabala wa Kiislamu. Watafitiwa walikuwa watunzi wa mashairi, waimbaji, wapiga ala za muziki pamoja na washabiki/wapenzi wa muziki wa taarab. Uchambuzi wa data umeonesha kuwa ni kweli kabisa kwamba pana usasa wa waziwazi kwenye mashairi katika taarab ya sasa. Usasa huo ndio msingi uliyoshusha hadhi ya mashairi ya taarab ya sasa na kuwa maneno tu. Vile vile, muziki huo utambulikanao kama taarab ya sasa wakosa vigezo thabiti vyenye kuyakinisha uhalali wa kuitwa taarab.
dc.format application/pdf
dc.language other
dc.publisher The State University of Zanzibar (SUZA)
dc.title Usasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa:
dc.title Fani na Maudhui
dc.type Thesis


Files in this item

Files Size Format View

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account