Description:
Poetry is a literary work which, as other genres of literature, performs two main functions in the society, educating and entertaining. In so doing, poetry, like philosophy, questions existing concepts and ideas, clarifies them, critically analyses those concepts and ideas and formulates a world view in a logical manner. Also, poetry, just like philosophy, is filled with wisdom which if accepted and utilized by the society, is likely to enhance socio-economic and political development. This paper is of the view that what philosophy and poetry do is similar to the extent that philosophy and poetry can be treated the same. That is to say, poets are philosophers of some kind. To present that, the paper analyses philosophical values of Muzale’s Nakuomba poems.
Ushairi ni kazi ya fasihi ambayo, kama tanzu nyingine za fasihi, una dhima kuu mbili katika jamii, kuelimisha na kuburudisha. Katika kutimiza dhima hizo, ushairi, kama ilivyo falsafa, huhoji dhana na mawazo yaliyopo, hufafanua, na kuhakiki dhana na mawazo yaliyopo katika jamii, na huunda mtazamo mpya wenye mantiki zaidi. Aidha, ushairi, kama tu ilivyo falsafa, umejaa mambo mbalimbali ya busara ambayo kama yatakubaliwa na kutekelezwa na jamii, yanaweza kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Makala haya yanaibua hoja kuwa ushairi na falsafa zina majukumu yanayofanana sana katika jamii kiasi kwamba ushairi na falsafa huweza kuchukuliwa kama vitu vinavyofanana sana. Hii ni kusema kuwa, washairi ni wanafalsafa kwa namna fulani. Ili kubainisha hilo, makala yanachambua masuala mbalimbali ya kifalsafa yanayobainika katika mashairi yaliyomo katika diwani ya Muzale ya Nakuomba.