Tamthiliya hii ya Rais wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni jaribio la kuiandika historia ya nchi ya Tanganyika (Tanzania) kwa njia ya kisanaa. Ni jaribio la kutaka kuongeza mchango wa kazi za kisanaa zinazozungumzia harakati za nchi ya Tanganyika tangu pale mkoloni alipokuwa akiitawala hadi ilipozaliwa upya Disemba 1961. Vilevile, tamthiliya hii inaonesha mchango wa wanaharakati mbalimbali ambao kwa matendo yao waliwezesha leo hii kuwa na taifa huru la Tanzania. Mchango wa watu kama Bibi Titi Mohamed hautajwi katika masomo ya historia ambayo tulijifunza shule ya msingi na sekondari. Mambo haya yanapaswa kurekebishwa ili vizazi vijavyo viijue historia ya nchi yetu kwa ufasaha.
Hii ni tamthiliya (mchezo wa kuigiza) unaosawiri historia ya nchi ya Tanganyika kwa njia ya kisanaa na kifasihi. Inahusu namna wapigania uhuru walivyojitoa muhanga ili kuhakikisha uhuru wa Tanganyika unapatikana. Hisoria hii inajumuisha vipindi mbalimbali ambavyo nchi ya Tanzania imepitia ikiwamo vita vya Kagera. Unaweza kununua nakala ya tamthiliya hii katika anwani ifuatayo:http://www.lulu.com/author/content_revise.php?fCID=18861610