COSTECH Integrated Repository

Mitindo ya Lugha katika Tovuti za Serikali Nchini Tanzania na Athari zake katika Usambazaji wa Taarifa kwa Umma

Show simple item record

dc.creator Kidami, Rhoda P.
dc.date 2021-04-27T15:40:33Z
dc.date 2021-04-27T15:40:33Z
dc.date 2019
dc.date.accessioned 2021-05-07T11:36:42Z
dc.date.available 2021-05-07T11:36:42Z
dc.identifier 0856-552X
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.11810/5685
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.11810/5685
dc.description Tovuti ni miongoni mwa vyanzo vinavyotumiwa na serikali ya Tanzania kusambaza taarifa kwa jamii. Lugha rasmi, yaani Kiswahili na Kiingereza, ndizo zinazotumiwa kwa usambazaji huo. Baadhi ya tovuti zina sehemu ya kuchagua lugha, hivyo, mtumiaji ana uhuru wa kuchagua lugha mojawapo kati ya hizo mbili. Katika makala hii tumechunguza jinsi lugha hizo zinavyotumiwa kwa pamoja kusambaza taarifa kwa umma wa Tanzania na duniani kote kwa ujumla. Kurasa za Kiswahili na za Kiingereza zilizomo ndani ya tovuti moja zimechunguzwa na kubainisha mitindo ya lugha inayotumiwa kisha kutathmini athari za mitindo hiyo katika usambazaji wa taarifa kwa umma. Uchunguzi huo umeongozwa na Mkabala wa Reh (2004) unaohusu aina za maandishi ya kijamiilughaulumbi katika jamii zenye wingilugha. Data zilikusanywa kutoka katika tovuti za wizara za serikali ya Tanzania. Tovuti zilizohusishwa ni zile zenye sehemu ya uchaguzi wa lugha ili kuwezesha ulinganishi wa matumizi ya lugha kati ya kurasa za Kiswahili na zile za Kiingereza. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha matumizi ya lugha mseto kati ya Kiswahili na Kiingereza yaliyopo katika mtindo wa ujalizaji. Mtindo huu ni faafu kwa watumiaji wenye uelewa wa lugha zote mbili ilhali kwa wenye uelewa wa lugha moja, yaani Kiswahili au Kiingereza, watapata baadhi tu ya taarifa.
dc.description Self
dc.language sw
dc.publisher TUKI
dc.relation Vol. 17;No. 1
dc.title Mitindo ya Lugha katika Tovuti za Serikali Nchini Tanzania na Athari zake katika Usambazaji wa Taarifa kwa Umma
dc.type Journal Article, Peer Reviewed


Files in this item

Files Size Format View

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account