Mabadiliko ya kasida: dhima na uwasilishaji
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Description
Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
Utafiti huu ulilenga kuchunguza mabadiliko ya kasida katika dhima na uwasilishaji wake Zanzibar ambao ulifanyika katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza mabadiliko ya kasida katika jamii ya Zanzibar katika dhima na uwasilishaji wake. Malengo mahsusi yalikuwa ni kutambulisha mabadiliko ya dhima yaliyojitokeza katika kasida za Kiswahili zinazotumiwa na jamii ya watu wa Zanzibar, kubainisha mabadiliko katika uwasilishaji wa kasida za Kiswahili zinazotumiwa na jamii ya Zanzibar pamoja na kuona athari za mabadiliko hayo. Mtafiti alitumia utaratibu wa uwandani na wa maktabani ambao ulitumia njia ya upekuzi wa marejeleo, uchunguzi shirikishi pamoja na usaili. Jumla ya kasida ishirini zilizilifanyiwa utafiti wa kina pamja na watafitiwa hamsini wakiwemo wazazi, walimu pamoja na wanafunzi wa madrasa. Nadharia ya Ubadilikaji Taratibu ndiyo iliyomuongoza mtafiti katika uchanganuzi wa data hizo zilizoteuliwa. Utafiti umeonesha kuwa yapo mabadiliko mbali mbali ya kasida katika uwasilishaji wa kasida pamoja na maudhui ya kasida katika jamii ya Wazanzibari na kwamba kasida husomwa kulingana na muktadha au matukio mbali mbali yanayojitokeza katika jamii husika. Pia utafiti uligundua kwamba kasida za Kiswahili zina nafasi nzuri katika kujenga maadili ya jamii husika kwani zimejikita karibu katika kila nyanja ya maisha ya Mzanzibari. Utafiti huu umeshauri jamii pamoja na wadau mbali mbali kuendeleza na kulinda hadhi ya kasida ili kuweza kutunza maadili ya jamii ya watu wa Zanzibar.

Keywords
Kasida, Mabadiliko ya kasida, Dhima, Dhima ya kasida, Uwasilishaji, Uwasilishaji wa kasida, Zanzibar, Mjini Magharibi Unguja