Suala la utendaji katika michezo ya jadi ya watoto: mfano kutoka Bumbwini- Zanzibar

No Thumbnail Available

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Description

Tasnifu (Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Jamii Katika Fasihi)
Utafiti huu umechunguza Utendaji Katika Michezo ya Jadi ya Watoto wa Bumbwini, Zanzibar. Tasnifu hii ilizingatia dhana kwamba kuna mtazamo finyu katika jamii kuhusiana na michezo ya watoto. Kuna wazo kuwa jamii imechukulia michezo ya jadi ya watoto kuwa ni kuwaburudisha na kuwapa mazoezi ya kimwili na kiakili tu. Kwa hivyo, utafiti huu umekusudia kubainisha dhima za utendaji katika michezo ya jadi ya watoto ili kuondoa dhana potofu ya jamii kuhusiana na michezo hiyo. Katika kukamilisha lengo la utafiti, ukusanyaji wa data wa uwandani ulitumika ili kuipata michezo kutoka katika sehemu husika inapochezwa. Usaili, hojaji na ushuhudiaji ni mbinu ambazo zilitumika katika utafiti huu. Michezo mingi ilitafitiwa ili kupata matokeo yaliyosahihi. Utafiti umeongozwa na nadharia ya Uamilifu ambayo inahusiana na kipande kazi cha kazi ya fasihi jinsi kinavyoweza kufanyakazi katika jamii. Nadharia ya uamilifu inazingatia matakwa ya jamii kulingana na uhusiano uliopo katika jamii husika na jinsi fasihi inavyofanyakazi. Nadharia hii imesaidia kubainisha michezo, miundo ya michezo na hatimae kubainisha dhima mbalimbali zilizojitokeza katika utendaji wa michezo ya watoto. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa kuna dhima nyingi zinazotekelezwa katika michezo ya jadi ya watoto. Dhima zimebainika kutokana na nadharia iliyotumika ambayo imejikita katika kuiangalia jamii na matakwa yake katika maisha ya kila siku. Utafiti umebaini kuwa michezo ya watoto inawakilisha matendo ya kila siku ya wanajamii na ambayo yanasawiri majukumu ya watu katika jamii husika. Kwa hivyo, utafiti umefuta dhana ya kuwa michezo ya watoto ni kupoteza muda au kuwaburudisha watoto tu.

Keywords

Michezo, Jadi, Watoto, Jadi ya watoto, Bumbwini, Zanzibar

Citation