dc.description |
Utafiti huu unahusu usawiri wa mwanamke katika hadithi za magazeti ya udaku.
Katika kufanikisha utafiti huu, hadithi tano ziliteuliwa ambazo ni Golden Tears
“Machozi ya Dhahabu”, “Wakili wa Moyo”, “Chichi wa Michepuko”, “Usiku wa
Kigodoro‟ na “My Repentance” (Kutubu Kwangu). Katika utafiti huu jamii ya
watafitiwa ni wasomaji wa magazeti ya udaku, wahariri, wauzaji, na watunzi wa
hadithi za kwenye magazeti hayo. Utafiti huu umefanyika katika mikoa mitatu
ambayo ni Iringa, Dodoma na Dar es Salaam. Aidha utafiti umehusisha watafitiwa
15. Ukusanyaji data umefanyika uwandani na maktabani. Data za uwandani
zimehusisha watu 15 ambao ni wasomaji wa hadithi, watunzi, wahariri na wauzaji
wa hadithi hizo. Mtafiti alipata data za ziada maktabani kupitia maandiko
mbalimbali. Data hizo zinahusu kufahamu watu wengine wamefanya nini kuhusu
mwanamke katika fasihi.
Ili kupata data hizo, mtafiti alitumia mbinu ya kudurusu matini, mahojiano na
majadiliano. Mbinu hizi zote zimekidhi haja za matakwa ya data zilizotakiwa na
utafiti huu. Utafiti huu umeongozwa na mkabala wa ufeministi ambao kwa hakika
umesaidia katika kuchambua data na mwisho kupata matokeo ya utafiti.
Utafiti huu umebaini kuwa mwanamke anasawiriwa katika hadithi za kwenye
magazeti ya udaku kama mtu malaya, mwenye mapenzi ya kweli na uongo, mbunifu
na chombo cha starehe. Dharimira hizi zinazomsawiri mwanamke zina athari chanya
na hasi katika jamii. Pia utafiti umebaini kuwa wasomaji wa hadithi hizi wa maoni
mbalimbali juu ya hadithi hizo miongoni mwa maoni hayo ni waandishi wabadili
mtizamo katika kumuumba mhusika mwanamke, badala ya kuumba kwa mtizamo
hasi tu sasa aumbwe kwa mtizamo chanya. |
|