COSTECH Integrated Repository

Athari za sayansi na teknolojia katika hadithi za watoto: mifano ya ngano kutoka wilaya ya Micheweni Pemba

Show simple item record

dc.creator Mbarouk, Mbarouk Juma
dc.date 2019-08-21T09:23:01Z
dc.date 2019-08-21T09:23:01Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:34Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:34Z
dc.identifier Mbarouk, M. J., (2015). Athari za sayansi na teknolojia katika hadithi za watoto: mifano ya ngano kutoka wilaya ya Micheweni Pemba. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma.
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/1047
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/1047
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Jamii katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Utafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza hadithi za watoto, kwa kuangalia jinsi hadithi hizo zilivyoathiriwa na maendeleo ya sasa ya sayansi na teknolojia. Hususan, kwa kuchunguza mifano ya hadithi za ngano kutoka Wilaya ya Micheweni Zanzibar. Utafiti ulibaini kwamba, sifa nyingi za Fasihi Simulizi zimebadilika au zimo katika mabadiliko makubwa. Hasa hasa katika kipindi hiki cha kukua na kuimarika kwa sayansi na teknolojia. Ikiwa hivyo ndivyo, basi ni dhahiri kwamba Fasihi Simulizi na vipera vyake inafaa vizidi kuchunguzwa zaidi, ili kujua ni kwa namna gani vipera hivyo vimeathiriwa na maendeleo hayo ya sayansi na teknolojia. Utafiti huu umeongozwa na malengo matatu, ambayo ni kuchunguza madhara yanayotokana na sayansi na teknolojia jinsi yanavyoathiri usimuliaji na uhifadhi wa hadithi za watoto, hususan hadithi za ngano, kutathmini mchango wa sayansi na teknolojia katika maendeleo ya utanzu wa hadithi za watoto, kwa kuangalia mifano ya ngano kutoka Wilaya ya Micheweni Zanzibar na lengo la tatu ni kuchunguza mwamko wa wanajamii wa Wilaya ya Micheweni walioupata kuhusiana na athari ya sayansi na teknolojia katika utanzu wa hadithi za watoto, kwenye mifano ya hadithi za ngano. Katika malengo matatu hayo kila lengo lilipewa nafasi kutegemea na matokeo ya utafiti wenyewe. Katika tasnifu hii, mkabala uliotumika ni wa nadharia ya Uhalisia. Nadharia hii imekuwa na umuhimu mkubwa sana katika kupata matokeo bora ya utafiti huu. Kwani nadharia hii ya uhalisia imetusaidia katika kujiridhisha kwamba, kila lengo tulilolijadili linasawiri uhalisi uliopo katika jamii ambayo ililengwa kufanyiwa utafiti. Matokeo ya utafiti huu ni kwamba, utatoa mchango mkubwa katika uga huu wa Fasihi Simulizi kwani ni sehemu muhimu ya chanzo cha taarifa za kifasihi. Utafiti huu unategemewa pia kuwa na faida kubwa kwa taifa, kwani utasaidia kufafanua hadithi za watoto, kwa kuangalia mifano ya ngano ambazo, kwa kiasi fulani, zinaelekea kupotea kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Pia utasaidia kuzifanya hadithi hizo zisambae na kufahamika na watu wengi ndani na nje ya nchi yetu.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Athari
dc.subject Athari za sayansi
dc.subject Athari za teknolojia
dc.subject Hadithi
dc.subject Ngano
dc.subject Michewani
dc.subject Pemba
dc.subject Teknolojia
dc.subject Hadithi za watoto
dc.title Athari za sayansi na teknolojia katika hadithi za watoto: mifano ya ngano kutoka wilaya ya Micheweni Pemba
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
MBAROUK JUMA MBAROUK.pdf 1.548Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account