dc.creator |
Haji, Gora Akida |
|
dc.date |
2019-08-28T09:24:16Z |
|
dc.date |
2019-08-28T09:24:16Z |
|
dc.date |
2015 |
|
dc.date.accessioned |
2022-10-20T13:54:34Z |
|
dc.date.available |
2022-10-20T13:54:34Z |
|
dc.identifier |
Haji, G. A. (2015). Upande wa pili wa riwaya teule za Shafi Adam Shafi: dhamira zilizofichama.Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma |
|
dc.identifier |
http://hdl.handle.net/20.500.12661/1203 |
|
dc.identifier.uri |
http://hdl.handle.net/20.500.12661/1203 |
|
dc.description |
Tasnifu (MA Kiswahili) |
|
dc.description |
Tasnifu hii ililenga kuchunguza Upande wa Pili wa Riwaya teule za Shafi Adam
Shafi” kwa kuangalia dhamira zilizofichama. Utafiti uliofaywa uliongozwa na
malengo matatu ambayo ni: Kuchunguza upande wa pili wa riwaya teule za Shafi A.
Shafi kwa kuangalia dhamira zilizofichama katika kazi hizo; Kuchunguza na
kubainisha miktadha mbalimbali iliyomsukuma Shafi A. Shafi kutumia mtindo huo
katika kazi zake hizo; na Kubainisha athari za mtindo uliotumika katika kazi za Shafi
A. Shafi kwa wasomaji wake.
Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni udurusu wa maktaba, usaili na
mahojiano ili kupata taarifa juu ya dhamira zilizofichama katika riwaya. Nadharia
zilizotumika katika utafiti huu wakati wa ukusanyaji na uchambuzi wa data ni nadharia
ya U-muundo na Umarx.
Matokeo ya jumla ya utafiti huu yalionesha dhamira zilizofichama katika kazi teule
kama zifuatazo: harakati za kupigania uhuru kuwa ngumu kutokana na vibaraka vya
kikoloni kufaidika na utawala huo, ushiriki wa wasomi katika harakati za kupigania
uhuru huo, kusalitiwa kwa wasomi baada ya kupatikana kwa uhuru huo pamoja na
suala la ukweli kuhusu harakati za mapinduzi ya Zanzibar.
Kutokana na matokeo haya, utafiti huu unashauri mambo yafuatayo: kwanza ni
kuzisoma kazi hizi kwa makini ili kuweza kubaini kwa kina juu ya mambo
yaliyofichama katika kazi hizi. Pili kazi hizi huweza kutumika kama rejea katika
kuijua historia ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla. |
|
dc.language |
Kisw |
|
dc.publisher |
Chuo Kikuu cha Dodoma |
|
dc.subject |
Riwaya |
|
dc.subject |
Riwaya za Shafi Adam Shafi |
|
dc.subject |
Shafi Adam Shafi |
|
dc.subject |
Dhamira |
|
dc.subject |
U-muundo |
|
dc.subject |
Umarx |
|
dc.subject |
Mitindo |
|
dc.title |
Upande wa pili wa riwaya teule za Shafi Adam Shafi: dhamira zilizofichama |
|
dc.type |
Dissertation |
|