COSTECH Integrated Repository

Matumizi ya msamiati unaosawiri mazingira ya kizanzibari katika riwaya za Muhammed Said Abdulla

Show simple item record

dc.creator Said, Saida Abdulla
dc.date 2019-08-29T11:08:13Z
dc.date 2019-08-29T11:08:13Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:35Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:35Z
dc.identifier Said, S. A., (2015). Matumizi ya msamiati unaosawiri mazingira ya kizanzibari katika riwaya za Muhammed Said Abdulla. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma.
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/1290
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/1290
dc.description Tasnifu (MA Kiswahili)
dc.description Tasnifu hii inahusu Matumizi ya msamiati unaosawiri mazingira ya Kizanzibari katika riwaya za Muhammed Said Abdulla. Msamiati ni jumla ya maneno yaliyomo katika lugha. Hivyo, kwa mujibu wa utafiti huu maneno yenyewe yalichunguzwa kupitia riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale, Duniani Kuna Watu na Kosa la Bwana Msa. Uchunguzi huu ulilenga kuchunguza na kubainisha msamiati huo na etimolojia yake pamoja na athari yake kwa wasomaji. Sababu ya kuchunguza suala hilo lilitokana na mtafiti kuvutika na lugha ya utunzi wa riwaya hizo. Shabaha ni kupunguza au kuondoa tatizo la kutofahamika maana iliyokusudiwa kwa baadhi ya msamiati, hasa kwa wale ambao si weledi wa kucheza na lugha hiyo. Mbinu ambazo zilitumika kupata data ni udurusu wa maandiko, udodosaji na mahojiano. Jamii tafitiwa katika uchunguzi huu ilikuwa ni ya Wazanzibari kwa kuwa ndiyo jamii ya mtunzi wa riwaya hizo. Data za uwandani zilizopatikana kwao zilichanganywa na zile za maktabani kupitia maandiko mbalimbali. Data hizi zilihusishwa na nadharia ya uhalisia kuhusu upatikanaji wa etimolojia sahihi ya msamiati unaosawiri mazingira ya Kizanzibari na matukio ambayo yamo katika riwaya za mtunzi huyo ambayo yamekithiri msamiati huo. Matukio ya uchunguzi huo yalibaini kuwa usawiri wa msamiati na mazingira ya Kizanzibari katika riwaya za Muhammed Said Abdulla upo kwa kiwango kikubwa. Usawiri huo ulibainika zaidi kupitia miktadha ya maisha ya Wazanzibari kijiografia, kilugha, kisanaa na kiutamaduni. Aidha, msamiati uliobainika ulijikita katika vipengele vya kihistoria (kupitia lugha ya Kiarabu na Kiingereza), kiutamaduni (kupitia utamaduni wa dini ya Kiislamu), na kilahaja (kupitia vijilugha vya wakazi wa Zanzibar). Hali hiyo imetoa athari kwa wasomaji ya kuvutika na uandishi wa mtunzi huyo, kubaini historia na silika yake, kubaini umahiri wake wa matumizi ya visawe, kubaini historia na athari ya Wakoloni, kutambulisha lahaja na utofauti wake kimatumizi, kushajiisha matumizi ya msamiati uliopo hatarini kupotea, na kuathiri watunzi wengine wa Zanzibar waliomfuatia. Pia matokeo ya uchunguzi huo yametoa mchango mpya kwa kuorodhesha msamiati na asili zake katika riwaya hizo.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Msamiati
dc.subject Usawiri
dc.subject Usawiri wa mazingira
dc.subject Kizanzibari
dc.subject Riwaya
dc.subject Muhammed Said Abdulla
dc.subject Riwaya za Muhammed Said Abdulla
dc.subject Etimolojia
dc.subject Nadharia
dc.title Matumizi ya msamiati unaosawiri mazingira ya kizanzibari katika riwaya za Muhammed Said Abdulla
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
SAIDA ABDULLA SAID.pdf 1.338Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account