COSTECH Integrated Repository

Uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma: Mifano kutoka shule za msingi Tanzania

Show simple item record

dc.creator Stephano, Rehema
dc.date 2019-09-03T10:00:08Z
dc.date 2019-09-03T10:00:08Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:03Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:03Z
dc.identifier Stephano, R. (2015). Uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma: Mifano kutoka shule za msingi Tanzania (Tasnifu ya uzamivu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/1543
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/1543
dc.description Tasnifu ya uzamivu
dc.description Utafiti huu umechunguza uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania zinazotumia mchepuo wa Kiswahili, hasa kwa kujikita katika mtaala wa Kiswahili. Malengo mahususi yaliyoshughulikiwa na utafiti huu ni matatu. Malengo hayo ni kuchambua viakifishi vinavyotumiwa katika uandishi wa kitaaluma wa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania, kuchunguza makosa ya uakifishaji yanavyojitokeza katika kazi za wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania na kubainisha sababu mbalimbali za makosa ya uakifishaji kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania. Utafiti huu umetumia mbinu mseto katika kukusanya data. Vilevile, umetumia mkabala wa kiidadi na wa kitaamuli kuwasilisha na kujadili data. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba wanafunzi wa Shule za Msingi wanafundishwa na wanatumia viakifishi vichache. Viakifishi hivyo ni nukta, kiulizo, mkato na mshangao, huku vingine vikitumika mara chache. Pia, matokeo ya utafiti yameonesha kuwa wanafunzi hawawezi kuakifisha kazi zao kwa usahihi kwa sababu hawafundishwi uakifishaji kwa kina, marefu na mapana. Kwa hali hiyo, wanafunzi hao huandika sentensi bebanifu, sentensi tata na vipande sentensi. Kwa hiyo, utafiti huu unapendekeza uakifishaji kufundishwa kama mada inayojitegemea katika viwango vyote vya elimu, Shule za Msingi, Sekondari hadi Vyuo Vikuu, ili wanafunzi waweze kuzielewa sheria na kanuni za uakifishaji na hivyo kuboresha maandiko yao ya kitaaluma.
dc.publisher The University of Dodoma
dc.subject Uandishi wa kitaaluma
dc.subject Viakifishi
dc.subject Shule za msingi
dc.subject Tanzania
dc.subject Uzingatizi
dc.subject Makosa ya uakifishaji
dc.subject Uchambuzi wa viakifishi
dc.title Uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma: Mifano kutoka shule za msingi Tanzania
dc.type Thesis


Files in this item

Files Size Format View
STEPHANO, REHEMA.pdf 2.350Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account