dc.description |
Utafiti wa tasnifu hii ulichunguza mdhihiriko wa mwendo katika ushairi wa Kiswahili huku mifano ikitolewa katika diwani ya Wasakatonge na Kimbunga zilizotungwa na Mohammed S. Khatib na Gora Haji Gora. Mwendo katika ushairi wa Kiswahili ni kipengele cha kifani kinachotumiwa na watunzi kuboresha utunzi wa kazi za kifasihi na kudhihirisha ubingwa wa mtunzi katika kusana kazi zao. Hata hivyo, kipengele hiki cha mwedo hakijashughulikiwa sanakwa upande wa mashairi ukilinganisha na riwaya na tamthilia. Hivyo, mtafiti aliona ipo haja ya kukishughulikia.Kwa kiasi kikubwa, utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Data za uwandani zimepatikana kwa mahojiano ya sampuli iliyoteuliwa Data zilikusanywa katika mji wa Zanzibar. Mbinu ya maelezo ndiyo iliyotumika katika kutolea matokeo ya utafiti huu. Uchambuzi wa data umefanywa kwa kutumia nadharia ya upokezi kutokana na mihimili yake kufaa katika kubainisha aina, dhima na athari zake ukilinganisha na diwani teule na kufafanua miktadha mbalimbali inayohusiana na mwendo uliomo katika diwani hizo.
Utafiti umebaini kuwa matokeo ya utafiti yanakwenda sambamba na malengo ya tasnifu hii kwa kuonesha usawiri wa vipengele vya mwendo, dhima na athari zake. Vipengele vilivyoibuliwa ni lugha, muundo, vina, wizani, maudhui, uteuzi wa maneno, mandhari na wakati, lafudhi, taswira, kibwagizo na maghani. Kwa upande wa dhima zilizojadiliwa ni pamoja na kutia hamasa za usomaji, kuibua hisia kwa wasomaji, kupendezesha mtu kusikiliza, kumpa uhuru mtunzi, kudhihirisha matumizi ya takriri, kujenga uwezo wa kufikiri, kuibua taharuki, chanzo cha kuibua maudhui, kuweka wazi nafasi ya mahadhi, kuonesha upekee wa mwandishi, mwendo kama kipengele cha kifani. Athari zimegawika katika sehemu mbili ambazo ni athari chanya zinazotokana na mwendo wa mashairi na athari na hasi. Athari chanya zilikuwa kama kufikisha ujumbe, kuleta uvuto kwa hadhira, kuleta msisimko, na kuchochea ukuaji wa lugha. Vile vile kwa upande wa athari hasi zilikuwa ni taaluma ndogo kwa hadhira, taaluma ndogo kwa waandishi, kuichosha hadhira na kupoteza taharuki. Mwisho mchango mkubwa wa utafiti huu ulibaini kuwepo kwa mwendo wa katika uga wa ashairi na hata katika ushairi wa Kiswahili. |
|