COSTECH Integrated Repository

Msukumo wa jamii katika mabadiliko ya utendaji wa tamthilia ya kiswahili

Show simple item record

dc.creator Faustine, Stella
dc.date 2022-03-08T11:50:11Z
dc.date 2022-03-08T11:50:11Z
dc.date 2020
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:53:50Z
dc.date.available 2022-10-20T13:53:50Z
dc.identifier Faustine, S. (2020). Msukumo wa jamii katika mabadiliko ya utendaji wa tamthilia ya kiswahili. Jarida la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili JUZ, 39(96-111)
dc.identifier URL: https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/4026
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/3460
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/3460
dc.description Ikisiri. Makala kamili inapatikana https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/4026
dc.description Tafiti mbalimbali zimekuwa zikijadili kuhusu tamthilia ya Kiswahili kwa kuangalia historia, maendeleo yake pamoja na vipengele vinavyounda utanzu huo kwa jumla. Vipengele vingine hasa vya mabadiliko ya utendaji wa tamthilia pamoja na msukumo wa kijamii katika kuzua mabadiliko hayo havikupewa kipaumbele. Hali hii imesababisha mabadiliko ya utendaji wa sanaa mbalimbali za maonyesho kama vile tamthilia, kutohusishwa na mabadiliko ya jamii, hivyo kusababisha ugumu katika kuelewa maudhui yaliyomo ndani yake kwa kina. Makala haya yanalenga kuziba pengo hilo kwa kuonesha namna msukumo wa jamii hususan uvumbuzi wa sayansi na teknolojia unavyochangia mabadiliko ya utendaji wa tamthilia. Makala yametumia data za maktabani ambazo zilipatikana kupitia njia ya udurusu wa nyaraka, mapitio ya tamthilia zilizohifadhiwa katika mfumo wa kidijiti, na usomaji makini wa tamthilia andishi. Data zilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli ambao hutumia maelezo katika uwasilishaji wa maudhui. Aidha, Nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti. Makala yamebainisha kuwa mabadiliko yaliyotokea katika jamii kama vile maendeleo ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, yana mchango mkubwa katika mabadiliko ya utendaji wa tamthilia. Kimsingi, makala yanatoa hamasa kwa waandishi na wahakiki wa tamthilia ya Kiswahili katika kuyahusisha maendeleo ya tamthilia na mabadiliko ya jamii
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
dc.subject Tamthilia kiswahili
dc.subject Mabadiliko utendaji tamthilia
dc.subject Msukumo jamii
dc.subject Udurusu nyaraka
dc.subject Tamthilia mapitio
dc.subject Nadharia uhalisia
dc.subject Sayansi teknolojia uvumbuzi
dc.title Msukumo wa jamii katika mabadiliko ya utendaji wa tamthilia ya kiswahili
dc.type Article


Files in this item

Files Size Format View
Faustine, Stella .pdf 6.354Kb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account