Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
Tasnifu hii inahusu Methali za Kiswahili Zilizoachwa: Sababu na Athari zake kwa Jamii. Methali za Kiswahili zilizoachwa ni semi zenye muhutasari wa mawazo ya busara kwa mkato zinazotokana na jamii ya Waswahili ambazo, kwa sasa hazitumiki tena. Methali hizo zilichunguzwa katika jamii ya Waswahili waishio Zanzibar ambayo katika utafiti huu inajulikana kwa jina la jamii ya Wazanzibari. Utafiti ulilenga kuzibainisha baadhi ya methali hizo, kuchunguza sababu na athari za kuachwa kwake katika jamii hiyo. Sababu ya kuchunguza suala hilo ilitokana na mtafiti kubaini baadhi ya methali hizo ambazo zilimvutia na kuona kuachwa kwake ni hasara kwani jamiii itapoteza vitu muhimu. Hivyo, shabaha ya kufanya utafiti huu nikuibua upya matumizi ya methali hizo ili jamii iweze kufaidika na hekima, falsafa, mafunzo na mvuto wake.
Mbinu zilizotumika kupata data ni udurusu wa maandiko, udodosaji, mahojiano na mjadala wa kikundi. Jamii tafitiwa ni ya Wazanzibari kwa kuwa ndiko ulikofanywa utafiti huu. Data zilizopatikana kutoka uwandani zilichanganywa na zile za maktabani.Nadharia ya Uamilifu yenye msingi wa kuangalia kazi ya fasihi simulizi ilitumika.
Matokeo ya utafiti yamebainikuwepokwa methali zilizoachwaambazo baadhi yake zimeoneshwa katika tasnifu hii. Pia,zipozinazotumiwa sana,kwa wastani na kwa nadra.Sababu za kuachwa methali hizo ni mvuvumko wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, ukosefu wa taasisi za kuzihifadhi na kuzirithisha, mabadiliko ya msamiati uliotumika katika methali hizo, na kuibuka kwa methali nyingi mpya.Athari chanyakwa jamii, ni kuondoka kwa msamiati mgumu usiotumika sasa,na kuiruhusu lugha kuwa na mabadiliko chanya ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. Kwa upande wa athari hasi ni kufifia kwautamaduni wa Wazanzibari, jamii kuzikosa adili za methali hizo, na jamii kukosa burudani itokanayo na methali hizo.Kwa matokeo hayo, utafiti huu ni muhimu kwa walimu, wanafunzi, wataalamu, na jamii nzima ya Wazanzibari na Waswahili kwa jumla.Tasnifu hiiina sura tano za ripoti ya utafiti,marejeleo pamoja na baadhi ya viambatisho vya utafiti huu.