dc.description |
Utafiti huu ulichunguza ‟Matumizi ya Lugha Katika Muziki wa Kizazi Kipya: Mifano Kutoka Katika Nyimbo za Mapenzi za Wasanii Inspekta Haroun na Mwanafalsa‟. Utafiti ulilenga kubainisha lugha inayotumika katika kusawiri vionjo vya mapenzi, katika nyimbo za wasanii teule wa muziki wa kizazi kipya; kuchunguza sababu zilizowafanya wasanii teule kutumia lugha hiyo katika kusawiri vionjo vya kimapenzi katika nyimbo zao; pamoja na kuchunguza athari ambazo hadhira hupata kutokana na matumizi ya nyimbo zinazobeba dhana ya mapenzi katika jamii. Mbinu ya ufafanuzi ndiyo ilitumika katika utafifiti huu wa kitaamuli huku nadharia ya Umuundo ndiyo iliyotumika katika uchambuzi wa data. Wakati mbinu za ukusanyaji data zilizotumika katika kuukamilisha utafiti huu ni udurusu wa kimaktaba, ushuhudiaji, usaili wa watafitiwa pamoja na mjadala wa vikundi.
Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa matumizi ya lugha katika muziki wa kizazi kipya, hususani katika tungo za mapenzi, hutumiwa na wasanii kutokana na sababu mbalimbali kama vile soko la muziki, mapenzi ya wasanii katika tungo hizo na hata kuonesha hisia zao kwa wapendwa wao.Tija zipatikanazo kutokana na utafiti huu ni kuburudisha jamii, kuongeza msamiati wa lugha, kudumisha mahusiano katika jamii. Pia, kuna athari zilizooneshwa kutokan na matumizi ya nyimbo zenye vionjo kama vile kujiingiza katika mahusiano katika umri mdogo, mmomonyoko wa maadili katika jamii na kudumaza kwa ubunifu. Mchango mpya ulioibuliwa na utafiti huu ni kuwepo/kuibuliwa kwa misimu mbalimbali ambayo inazungumzia mapenzi au huonesha vionjo vya mapenzi katika jamii. Vilevile, kwa kupitia utafiti huu nyimbo teule za mapenzi pamoja na taarifa za wasanii hawa wateule zitaweza kuhifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye na watafiti wengine pindi zitakapohitajika |
|