COSTECH Integrated Repository

Ujumi katika muziki wa dansi: mfano kutoka nyimbo teule za Marijani Rajabu na Ally Choki

Show simple item record

dc.creator Laswai, Agripina
dc.date 2019-01-18T09:47:01Z
dc.date 2019-01-18T09:47:01Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:32Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:32Z
dc.identifier Laswai, A. (2015). Ujumi katika muziki wa dansi: mfano kutoka nyimbo teule za Marijani Rajabu na Ally Choki. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/544
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/544
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Tasnifu hii ni matokeo ya utafiti uliojigeza katika kuchambua vipengele vya kiujumi katika muziki wa dansi wa wanamuziki wawili Marijani Rajabu na Ally Choki. Utafiti ulilenga kuchunguza ujumi katika muziki wa dansi wa Tanzania ili kuthibitisha kuwa taaluma ya ujumi ina nafasi kubwa katika kazi za muziki wa dansi. Pia tasnifu hii imejaribu kuona ni kwa kiasi gani, kazi hizo zenye mwelekeo wa kiujumi zinafungamana na idili za jamii ya Watanzania. Aidha imejaribu kutathimini dhima ya vipengele vya kiujumi katika fani na maudhui ya nyimbo za wanamuziki teule. Njia zilizotumika kukusanya data ni kutalii uwandani na udurusi wa kimaktaba. Uchambuzi wa data ulifanywa kwa njia ya ufafanuzi. Data zilizopatikana ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo, halikadhalika, vielelezo vilitumika kwa kiasi kidogo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Kimarx. Nadharia ya Kimarx imetoa mwongozo wa kuchunguza utamaduni na maisha ya watu weusi kwa ujumla. Matokeo ya utafiti huu yameleta mchango mpya wa kitaaluma katika Fasihi ya Kiswahili. Tasnifu imebainisha kuwa uzuri hutambuliwa kwa namna tofauti kati ya jamii moja na nyingine, na ili kuyachambua vyema masuala ya kiujumi, hutupasa kujua idili za jamii husika.Tumebainisha muktadha wa utunzi wa muziki wa dansi kwa jamii ya wakati huu wa maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia. Miongoni mwa michango ni pamoja na matumizi ya idili, adabu na utiifu na umoja katika kufafanua uzuri wa kiujumi katika muziki wa dansi. Aidha, tumetathimini dhima ya vipengele vya kiujumi katika fani na maudhui ya nyimbo teule za Marijani Rajani na Ally Choki. Dhima hizo ni kuelimisha, kuburudisha, kutambulisha jamii na kuonyesha nafasi ya mwanamke katika jamii.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Lugha
dc.subject Ujumi
dc.subject Muziki
dc.subject Muziki wa dansi
dc.subject Nyimbo
dc.subject Marijani Rajabu
dc.subject Ally Choki
dc.subject Nadharia ya Kimarx
dc.title Ujumi katika muziki wa dansi: mfano kutoka nyimbo teule za Marijani Rajabu na Ally Choki
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
AGRIPINA LASWAI.pdf 1.069Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account