dc.description |
Utafiti huu ulilenga katika kuchunguza Dhima ya Nyimbo za Bongo Fleva
zihusuzo Rushwa katika kuleta Mabadiliko kwa Jamii. Bongo Fleva ni nyimbo
za kizazi kipya nchini Tanzania. Nyimbo hizi huwa na dhamira mbalimbali ambazo
hulenga kuelimisha na kuburudisha jamii inayokusudiwa na msanii. Njia ya nyimbo
huwa bora zaidi kwani huwafikia sehemu kubwa ya jamii. Kutokana na umuhimu wa
nyimbo jamii hupata mwitikio na kuifanya jamii kupata mabadiliko na kuifanya
jamii mpya yenye maadili mema. Nyimbo mara nyingi husadifu mazingira ya jamii
anapoimbia msanii na zinalenga vyema katika kutambulisha utamaduni wetu kwa
kuyaweka mambo yetu.
Utafiti huu uliongozwa na malengo ya aina mbili ambayo ni lengo la jumla la utafiti
ambalo lilikuwa kuchunguza dhima ya nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa kwa
mabadiliko ya jamii. Pia malengo mahususi matatu, Kwanza kukusanya nyimbo za
Bongo Fleva zihusuzo rushwa zinazoimbwa na wasanii mbalimbali katika Jamii, Pili
kuchunguza na kuainisha dhima zinazopatikana katika nyimbo za Bongo Fleva
zihusuzo rushwa, na Tatu kuchunguza mwitikio wa jamii kuhusiana na nyimbo za
Bongo Fleva zihusuzo rushwa.
Utafiti huu katika nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa tulizozisikiliza na
kuzitumia kama kifani chetu tulibaini dhima mbalimbali kama vile kuelimisha,
kuarifu, kukemea, kuadili, kuonya, ukombozi, kudhihaki uoga, kutia hamasa,
kupitisha amali za jamii na kutumika kama rekodi ya matukio muhimu katika jamii.
Utafiti huu ulifanyika maktabani na uwandani, maeneo mbalimbali ya halmashauri
ya jiji la Mbeya yalitumika katika kukusanya data. Nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo
rushwa zilikusanywa na kuwekwa katika maandishi, kisha kuchambuliwa na kupata
dhima zinazopatikana katika nyimbo kwa mabadiliko ya jamii. Mwitikio wa jamii
kuhusiana na nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa na mwisho mabadiliko
yaliyopatikana kutokana na nyimbo.
Uchambuzi wa data umefanywa kwa kutumia mkabala wa U-marx, Matokeo
yanaonesha U-marx unajikita katika kuleta mabadiliko kwa kujua historia ya jambo
na kuelewa tatizo kisha kuliunda upya kwa namna bora zaidi tofauti na awali. Pia
nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa zimewekwa katika maandishi. |
|