COSTECH Integrated Repository

Semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara: uchunguzi kuhusu asili, muundo, miktadha ya utokeaji na dhima

Show simple item record

dc.creator Shayo, Inocent Faustine
dc.date 2019-08-20T07:24:50Z
dc.date 2019-08-20T07:24:50Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:34Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:34Z
dc.identifier Shayo, I. F. (2015). Semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara: uchunguzi kuhusu asili, muundo, miktadha ya utokeaji na dhima. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/983
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/983
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Tasnifu hii inatokana na utafiti uliofanywa kuhusu semi zilizoandikwa katika maeneo mbalimbali ya biashara. Mambo ya msingi yaliyochunguzwa katika semi hizi ni asili, miktadha ya utokeaji, miundo na dhima. Utafiti huu ulifanyika katika mji wa Same mkoani Kilimanjaro. Semi za biashara ni semi ambazo hujitokeza katika muktadha wa kibiashara kwa kuandikwa au kutumiwa katika mazungumzo ya kila siku ya kibiashara japokuwa utafiti uliangalia semi zilizoandikwa tu. Malengo mahususi ambayo yameuongoza utafiti huu yalikua manne ambayo ni: kubainisha semi mbalimbali zilizoandikwa katika maeneo ya biashara, kuchunguza miundo ya semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara, kuchunguza miktadha inayohusiana na kuibuka kwa semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara, pamoja na kuchunguza dhima za semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara. Nadharia ya Mwitikio wa msomaji ndiyo iliyotumika kuuongoza utafiti huu. Nadharia hii imetumika kwa sababu inahimiza juu ya mchango wa msomaji, mtazamaji au mwonaji wa kazi ya fasihi na sio mwandishi. Wauzaji, wamiliki na wateja wa maeneo mbalimbali ya biashara walihojiwa na kutoa maoni yao juu ya dhima na asili ya semi hizo. Hivyo, ili kufikia malengo ya utafiti huu nadharia hii ndiyo inayokidhi haja. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data katika utafiti huu ni ushuhudiaji, udodosaji na maktabani. Vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji wa data ni hojaji, kamera, ngamizi (kompyuta), shajara na simu. Utafiti umebaini kuwa semi zilizoandikwa katika maeneo mbalimbali ya biashara zimebeba dhima kubwa ambazo huielezea jamii katika nyanja zote yaani kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Vilevile, semi hizi huwa na miundo mbalimbali na hazitegemei muundo mmoja katika uandikwaji wake. Aidha, semi hizi hujitokeza katika miktadha tofauti tofauti kutegemeana na kusudio au dhima iliyobebwa. Utafiti huu umesaidia kuonesha na kutambulisha faida, umuhimu, na nafasi ya semi ambazo huandikwa katika maeneo ya biashara.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Semi
dc.subject Biashara
dc.subject Asili
dc.subject Muundo
dc.subject Miktadha
dc.subject Dhima
dc.subject Dhima za semi
dc.subject Same
dc.subject Kilimanjaro
dc.title Semi zilizoandikwa katika maeneo ya biashara: uchunguzi kuhusu asili, muundo, miktadha ya utokeaji na dhima
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
INOCENT FAUSTINE SHAYO.pdf 2.091Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account