dc.creator |
Hemed, Bimkubwa Abdulrahman |
|
dc.date |
2019-08-20T08:29:34Z |
|
dc.date |
2019-08-20T08:29:34Z |
|
dc.date |
2015 |
|
dc.date.accessioned |
2022-10-20T13:54:34Z |
|
dc.date.available |
2022-10-20T13:54:34Z |
|
dc.identifier |
Hemed, B. A. (2015). Athari za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa nyimbo za watoto waishio Mijini. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma |
|
dc.identifier |
http://hdl.handle.net/20.500.12661/987 |
|
dc.identifier.uri |
http://hdl.handle.net/20.500.12661/987 |
|
dc.description |
Tasnifu ( Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili) |
|
dc.description |
Utafiti huu umechunguza namna Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
inavyoathiri nyimbo za watoto hususan maeneo ya mijini ambako maendeleo hayo
ya sayansi na teknolojia ndiko yanakopatikana kwa wingi.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Usosholojia iliyoasisiwa kwa kuja kupingana
na ulimbwende karne ya kumi na tisa. Utafiti huu umejumuisha mbinu ya mahojiano
na hojaji kukusanya data hatimaye imechanganuliwa kwa njia ya maelezo.
Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa maendeleo ya teknolojia ya habari na
mawasiliano yaliyopo nchini hususan mijini, yameathiri kwa kiasi kikubwa nyimbo
za watoto kutokana na kuwepo kwa vyombo vingi vya habari hapa nchini, ambao
ushindani wao wa kibiashara ndio unaowafanya warushe hewani nyimbo za wasanii
mbali mbali na kuacha zile za watoto ambapo watoto walikuwa wanaziimba kabla
yake.
Suala la msingi lililobainishwa na utafiti huu ni kwamba nyimbo za watoto
zimeathiriwa na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kutokana na matokeo ya utafiti huu, mapendekezo yafuatayo yamezingatiwa.
Serikali na jamii wafanye juhudi za makusudi kurejesha hadhi ya nyimbo za watoto
kwa kuziingiza katika mitaala ya shule pamoja na wazazi kufanya juhudi za
makusudi kuwafundisha nyimbo hizo ili zisiendelee kupotea. Pia, imependekezwa
tafiti zaidi zifanywe kuhusu tanzu mbalimbali za fasihi simulizi, na kwamba watafiti
wasikidharau kipengele hiki cha nyimbo za watoto kwani mbali na kutoa burudani,
pia watoto hupata mazoezi ya kutosha nakuwafanya wawe wakakamavu na wenye
afya. |
|
dc.language |
Kisw |
|
dc.publisher |
Chuo Kikuu cha Dodoma |
|
dc.subject |
Teknolojia ya habari na mawasiliano |
|
dc.subject |
TEHAMA |
|
dc.subject |
Nyimbo |
|
dc.subject |
Nyimbo za watoto |
|
dc.subject |
Mijini |
|
dc.subject |
Usosholojia |
|
dc.title |
Athari za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa nyimbo za watoto waishio Mijini |
|
dc.type |
Dissertation |
|