Athari za teknolojia katika Ngano

dc.creatorMbarouk, Maimuna Ali
dc.date2019-08-20T06:20:44Z
dc.date2019-08-20T06:20:44Z
dc.date2015
dc.date.accessioned2022-10-20T13:54:34Z
dc.date.available2022-10-20T13:54:34Z
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.descriptionUtafiti huu ulilenga kuchunguza Athari za Teknolojia katika Ngano, ambao uliongozwa na malengo matatu nayo ni kuchunguza historia ya ngano Zanzibar, kuchambua maendeleo ya teknolojia ambayo yanaathiri ngano na kubainisha athari za maendeleo ya teknolojia katika hadithi za ngano. Mbinu zilizotumika ili kuweza kutatua tatizo la utafiti ni udurusu wa kimaktaba, usikilizaji wa vyombo vya habari, mahojiano na mjadala wa vikundi. Sampuli ya watafitiwa ilikuwa ni wanafunzi, walimu kutoka SUZA, wakaazi wa mkoa wa Mjini Magharibi na wafanyakazi wa ZBC. Nadharia aliyotumia mtafiti katika uchambuzi wa data ni nadharia ya uhalisia ambayo ndiyo iliyomuongoza katika uchambuzi wa data. Matokeo yautafiti yanaonesha kuwa chimbuko la ngano ni kuwaasa watoto juu ya tabia ambazo hazikubaliki katika jamii, watu kujionesha kuwa wana vipawa vya kutumia lugha na pia ni watu kutaka kujionesha namna wanavyoyaelewa mazingira yao. Ngano ziliwasilishwa kwa mdomo. Maendeleo ya teknolojia ambayo yanatumika kuwasilishia, kuhifadhia, kusambaza ngano ni maandishi, CD, kanda za video na kanda za kunasia sauti pamoja na kompiyuta. Athari zinazopatikana kwa kutumia vifaa vya teknolojia katika kuwasilisha, kuhifahia na kusambazia ngano zimebainika kuwa zipo chanya na hasi. Mwishowe utafiti huu umetoa mapendekezo kuwa serikali kupitia wizara husika kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa ngano na pia kuzikusanya kwa ajili ya kuzihifadhi ili zisipotee moja kwa moja, teknolojia ambayo itatumika kuhifadhia ngano hizo iwe ni ya kudumu na kuigizwa ili zipate uasili wake na pia maskulini sisitumike kufundishia lugha tu bali iwe ni nyenzo ya wanafunzi kuvuna taaluma iliyomo katika ngano hizo.
dc.identifierMbarouk, M. A. (2015). Athari za teknolojia katika Ngano. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifierhttp://hdl.handle.net/20.500.12661/971
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/971
dc.languageKisw
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodoma
dc.subjectTeknolojia
dc.subjectNgano
dc.subjectHadithi
dc.subjectHadithi za ngano
dc.subjectZanzibar
dc.subjectAthari za teknolojia
dc.titleAthari za teknolojia katika Ngano
dc.typeDissertation

Files