Uhalisia wa maisha ya jamii ya wanyakyusa unavyosawiriwa katika dhamira za nyimbo za ngoma ya Maghosi

dc.creatorShuma, Clara
dc.date2019-08-18T10:28:25Z
dc.date2019-08-18T10:28:25Z
dc.date2015
dc.date.accessioned2022-10-20T13:54:33Z
dc.date.available2022-10-20T13:54:33Z
dc.descriptionTasnifu (Uzamili Fasihi ya Kiswahili)
dc.descriptionUtafiti huu ulichunguza uhalisia wa maisha ya jamii ya Wanyakyusa unavyosawiriwa katika nyimbo za ngoma ya Maghosi. Ngoma ya Maghosi ni ngoma ambayo huchezwa na jamii ya Wanyakyusa wanaoishi kwenye vijiji mbalimbali ambavyo vinapatikana katika wilaya ya Rungwe wakati wa kiangazi baada ya mavuno. Data zilikusanywa uwandani; ambapo mtafiti alikwenda katika mazingira halisi na kutumia mbinu ya kushuhudia na mahojiano. Uchambuzi na uchanganuzi wa taarifa zote zilizopatikana katika mchakato wa utafiti uliongozwa na nadharia ya Usosholojia na kuwasilishwa kwa kutumia mbinu ya ufafanuzi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba, nyimbo za ngoma ya Maghosi zimesheheni dhamira lukuki. Miongoni mwa dhamira hizo ni, uwajibikaji na kutowajibika kwa viongozi, umoja na mshikamano, unyonyaji, kuinua kipato cha wananchi, uaminifu katika ndoa, tahadhari ya magonjwa hatari, ndoa za kulazimishwa, suala la malezi, kutunza bikira na suala la mavazi. Aidha, utafiti umegundua kuwa dhamira zinazopatikana kwenye nyimbo hizo zinasawiri maisha halisi ya jamii ya Wanyakyusa kutokana na fasihi kuakisi yale yaliyotokea/yanayotokea katika jamii husika.
dc.identifierShuma, C. (2015). Uhalisia wa maisha ya jamii ya wanyakyusa unavyosawiriwa katika dhamira za nyimbo za ngoma ya Maghosi. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma.
dc.identifierhttp://hdl.handle.net/20.500.12661/775
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/775
dc.languageKisw
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodoma
dc.subjectMaisha ya wanyakyusa
dc.subjectWanyakyusa
dc.subjectNgoma za asili
dc.subjectNgoma ya maghosi
dc.subjectNyimbo za asili
dc.subjectTanzania
dc.subjectNadharia ya Usosholojia
dc.subjectMavuno
dc.subjectUnyonyaji
dc.subjectUaminifu
dc.subjectMalezi
dc.subjectUmoja
dc.titleUhalisia wa maisha ya jamii ya wanyakyusa unavyosawiriwa katika dhamira za nyimbo za ngoma ya Maghosi
dc.typeDissertation

Files