Nafasi ya mwanamke katika methali za Kikerewe

dc.creatorKakuru, Yovin Butega
dc.date2019-08-20T05:52:16Z
dc.date2019-08-20T05:52:16Z
dc.date2015
dc.date.accessioned2022-10-20T13:54:36Z
dc.date.available2022-10-20T13:54:36Z
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.descriptionTasnifu hii inahusu nafasi ya mwanamke katika methali za Kikerewe. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza nafasi ya mwanamke katika methali za Kikerewe ambazo hutumiwa katika shughuli zao za kifamilia. Data zilikusanywa uwandani na maktabani. Baada ya hapo, mtafiti alitumia mkabala wa maelezo, pamoja na nadharia ya Ufeministi katika kuchanganua data. Tasnifu hii imekusudia kuziba pengo linayojitokeza kwa kuchunguza nafasi ya mwanamke katika methali za Kikerewe. Kuweza kuzamia hasa katika matumizi ya methali hizo kwa mwanamke, namna methali hizo zinavyomchora mwanamke na hata pia athari za methali hizo kwa jamii. Udodosaji na mahojiano ni mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data zilizosaidia upatikanaji wa tasnifu hii. Utafiti huu ulibaini kuwa katika methali za Kikerewe zilizo nyingi, nafasi ya mwanamke kwa jamii hiyo ni ya kumdunisha. Hii ni kutokana na mfumo mzima wa maisha, mila, na desturi ambazo zimewakuza na ambazo ndicho kigezo kikubwa kinachowafanya watumie methali katika kumshambulia mwanamke na kuamini kuwa mwanamke ndiye chanzo cha matatizo ya kila jambo baya. Pia, tasnifu imeeleza nafasi ya mwanamke katika methali za Kikerewe kwa kujiegemeza katika methali kwa kumwangalia mwanamke, usawiri wa mwanamke katika methali na athari ya methali hizo kwa mwanamke. Mchango mpya wa tasnifu hii ni kwamba, elimu ni muhimu kwa mwanamke asiyetambua haki yake hasa kwa wale waishio vijijini.
dc.identifierKakuru, Y. B., (2015). Nafasi ya mwanamke katika methali za Kikerewe. Dodoma: Chuo kikuu cha Dodoma.
dc.identifierhttp://hdl.handle.net/20.500.12661/967
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/967
dc.languageKisw
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodoma
dc.subjectMwanamke
dc.subjectMethali
dc.subjectKikerewe
dc.subjectMethali za Kikerewe
dc.subjectUfeministi
dc.titleNafasi ya mwanamke katika methali za Kikerewe
dc.typeDissertation

Files