Suala la ufungwa katika ushairi wa kiswahili: mifano kutoka diwani za sauti ya dhiki na chembe cha moyo
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Description
Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili
Tasnifu hii inajadili suala la ufungwa katika diwani za Sauti ya Dhiki (1973) na Chembe cha Moyo (1988). Tatizo lililomsukuma mtafiti kufanya utafiti huu ni kwa kuwa tafiti katika uga huu wa ufungwa bado ni finyu. Kwa kutumia nadharia ya uhemenitiki na nadharia ya Ki-Marx mtafiti alichunguza suala la ufungwa katika ushairi wa Kiswahili kwa kutumia diwani teule. Data zilikusanywa maktabani na uwandani maeneo ya Zanzibar, Kenya, Dar es Salaam na Dodoma. Mbinu zilizotumika katika utafiti huu ni udurusu wa maktabani, njia ya udodosaji na njia ya mahojiano. Data zilichanganuliwa kwa kuzingatia njia ya maelezo ya utafiti pamoja na misingi ya nadharia za Uhemenitiki na Ki-Marx. Utafiti umegundua namna ufungwa ulivyokabiliwa na vikwazo vikubwa katika jamii inayohusiana na wafungwa. Kwa hivyo, utafiti umetoa mchango mkubwa kuhusiana na suala la ufungwa katika kipengele cha fasihi andishi ya Kiswahili kwa upande wa ushairi. Mchango mpya ulioibuliwa kutokana na utafiti ni huu ufuatao: Utafiti umegundua matatizo yanayowapata wafungwa wa aina yoyote katika jamii, kwa mfano, ufungwa wa gerezani, mfungwa anapowekwa gerezani huteswa na hukatiwa matumaini yake yote katika mustakbali wa maisha yake. Pia, kumpotezea malengo kwa watu waliomzunguka akiwa kama ni muhimili mkuu wa jamii hiyo ikiwemo familia. Tatizo hili linaweza kurekebishika. Wafungwa badala kuadhibiwa vikali magerezani wakatumiwa kama rasilimali watu kwa kutumia ujuzi walionao kunufaisha jamii na taifa kwa jumla. Aidha, utafiti umeonesha namna ambavyo nadharia za Uhemenitiki na Ki-Marx kwa kutumia misingi yake ilivyokuwa faafu kwa utafiti huu.

Keywords
Sauti ya dhiki, Chembe cha moyo, Ufungwa, Ushairi, Fasihi, Nadharia ya uhemenitiki, Nadharia ya Ki-Marx, Fasihi andishi, Mafunzo, Gerezani, Kiswahili, Familia, Nadharia