Dhima ya tamathali za semi katika nyimbo za siasa za Wagogo
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Description
Tasnifu (MA Kiswahili)
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kubaini dhima ya tamathali za semi katika nyimbo za siasa za Wagogo. Data zilikusanywa kutoka jamii ya kabila la Wagogo wanaoishi mkoa wa Dodoma, wilaya ya Kongwa kata ya Mtanana. Nyimbo mbalimbali za siasa zilikusanywa toka kwa wasanii mbalimbali wa kata ya Mtanana na kwa baadhi ya wananchi wa kata hiyo walihojiwa. Vilevile, zoezi la ushuhudiaji wa nyimbo za siasa ulifanywa na mtafiti. Aidha, mijadala mbalimbali ya vikundi ilifanywa. Nyimbo zilizokusanywa zilichambuliwa ili kuona jinsi tamathali za semi zinavyojitokeza, athari zake na dhima yake kwa jamii. Mbinu ya maelezo ilitumika katika kufanya utafiti huu na data zilichambuliwa kwa kutumia nadharia ya uhalisia wa kijamaa na nadharia ya U-Marx. Kadhalika, makala mbalimbali zilisomwa ili kupata data zinazohusiana na utafiti huu. Utafiti huu umebaini kuwa tamathali za semi zinazotumiwa na wasanii wa nyimbo za siasa toka katika jamii ya Wagogo hazitumiwi bure, bali zina dhima mahususi. Imebainika kuwa, tamathali za semi zinazojitokeza katika nyimbo za siasa za Wagogo zimejitokeza kwa namna mbalimbali zikiwa na dhima ya kuburudisha, kukosoa, kuokoa muda, kuhamasisha, kuweka msisitizo wa mambo, kuepusha migogoro, kuendeleza utamaduni na kujenga taswira. Utafiti huu ulibaini kuwa, wasanii wa nyimbo za siasa wamepevuka kisanaa kwani wanaweza kuweka vionjo vya kifasihi hasa katika matumizi ya lugha kwa kuweka tamathali za semi katika nyimbo zao kwa malengo maalum ambapo tamathali hizo za semi huleta athari mbalimbali kwa jamii.

Keywords
Dhima, Dhima ya tamathali, Tamathali za semi, Nyimbo, Nyimbo za siasa, Wagogo, Nyimbo za Wagogo