Usawiri wa mwanamke katika hadithi za magazeti ya udaku
dc.creator | Ngongolo, Mheza Juma | |
dc.date | 2019-08-21T09:04:00Z | |
dc.date | 2019-08-21T09:04:00Z | |
dc.date | 2015 | |
dc.date.accessioned | 2022-10-20T13:54:35Z | |
dc.date.available | 2022-10-20T13:54:35Z | |
dc.description | Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili) | |
dc.description | Utafiti huu unahusu usawiri wa mwanamke katika hadithi za magazeti ya udaku. Katika kufanikisha utafiti huu, hadithi tano ziliteuliwa ambazo ni Golden Tears “Machozi ya Dhahabu”, “Wakili wa Moyo”, “Chichi wa Michepuko”, “Usiku wa Kigodoro‟ na “My Repentance” (Kutubu Kwangu). Katika utafiti huu jamii ya watafitiwa ni wasomaji wa magazeti ya udaku, wahariri, wauzaji, na watunzi wa hadithi za kwenye magazeti hayo. Utafiti huu umefanyika katika mikoa mitatu ambayo ni Iringa, Dodoma na Dar es Salaam. Aidha utafiti umehusisha watafitiwa 15. Ukusanyaji data umefanyika uwandani na maktabani. Data za uwandani zimehusisha watu 15 ambao ni wasomaji wa hadithi, watunzi, wahariri na wauzaji wa hadithi hizo. Mtafiti alipata data za ziada maktabani kupitia maandiko mbalimbali. Data hizo zinahusu kufahamu watu wengine wamefanya nini kuhusu mwanamke katika fasihi. Ili kupata data hizo, mtafiti alitumia mbinu ya kudurusu matini, mahojiano na majadiliano. Mbinu hizi zote zimekidhi haja za matakwa ya data zilizotakiwa na utafiti huu. Utafiti huu umeongozwa na mkabala wa ufeministi ambao kwa hakika umesaidia katika kuchambua data na mwisho kupata matokeo ya utafiti. Utafiti huu umebaini kuwa mwanamke anasawiriwa katika hadithi za kwenye magazeti ya udaku kama mtu malaya, mwenye mapenzi ya kweli na uongo, mbunifu na chombo cha starehe. Dharimira hizi zinazomsawiri mwanamke zina athari chanya na hasi katika jamii. Pia utafiti umebaini kuwa wasomaji wa hadithi hizi wa maoni mbalimbali juu ya hadithi hizo miongoni mwa maoni hayo ni waandishi wabadili mtizamo katika kumuumba mhusika mwanamke, badala ya kuumba kwa mtizamo hasi tu sasa aumbwe kwa mtizamo chanya. | |
dc.identifier | Ngongoro, M.J., (2015). Usawiri wa mwanamke katika hadithi za magazeti ya udaku. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma. | |
dc.identifier | http://hdl.handle.net/20.500.12661/1043 | |
dc.identifier.uri | http://hdl.handle.net/20.500.12661/1043 | |
dc.language | Kisw | |
dc.publisher | Chuo Kikuu cha Dodoma | |
dc.subject | Usawiri | |
dc.subject | Mwanamke | |
dc.subject | Usawiri wa mwanamke | |
dc.subject | Hadithi | |
dc.subject | Hadithi za magazeti | |
dc.subject | Magazeti | |
dc.subject | Udaku | |
dc.subject | Magazeti ya udaku | |
dc.title | Usawiri wa mwanamke katika hadithi za magazeti ya udaku | |
dc.type | Dissertation |