Utani katika sherehe za harusi za watumbatu: aina, sababu na taashira zake
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Description
Tasinifu (Shahada ya Uzamili Sayansi ya jamii katika Fasihi ya Kiswahili)
Utafiti huu ulichunguza utani katika sherehe za harusi za Watumbatu. Utani ni chombo muhimu kinachowasilisha fikira, ujumbe na mwelekeo wa kijamii. Kwa kutumia utani jamii hutambulisha asili, utamaduni wake pamoja na kurithisha mila na silka za jamii. Watani hutupiana maneno yenye mzaha, kejeli, izara na hata matusi makali bila kuzingatia wale wanaowasikiliza, jambo ambalo baadhi ya hadhira hulalamikia jambo hilo. Utafiti huu ulifanyika katika kisiwa cha Tumbatu chenye shehia tatu ambazo ni Uvivini, Jongowe na Gomani. Watafitiwa walikuwa hamsini na watano (55).Mbinu zilizotumika katika utafiti huu ni udurusu, mahojiano, udodoshaji na ushuhudiaji. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya Uhemenitiki ambayo inaongozwa na msingi wa kufasiri matini kwa kuzingatia utukuzaji na ufufuaji wa maana za matini kimuktadha, kisaikolojia na kisarufi. Hivyo taashira zilizomo ndani ya utani ziligunduliwa kupitia misingi ya nadharia hii. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwapo kwa aina nne za utani ufanyikao katika sherehe za Watumbatu. Nazo ni utani wa binamu, utani wa mashemeji, utani wa babu/ bibi na wajukuu, na utani wa marafiki. Utani huo hufanywa kwa sababu ya kujitambulisha, kuonesha mahusiano, kufunza na kuburudisha. Aghalabu, utani huo ufanyikao katika sherehe za harusi hutamalakiwa na matumizi ya matusi na kejeli ambazo huwa na taashira maalumu iliyokusudiwa.Pia, utafiti uligundua na kubainisha taashira mbalimbali zinazotokana na utani kupitia maneno na matendo. Hii ni kwa sababu hutoa ujumbe maalumu unaopaswa kuzingatiwa na wanandoa na hata hadhira shiriki wa harusi hiyo. Hii ina maana kuwa utani una nafasi muhimu katika jamii.

Keywords
Utani, Sherehe, Sherehe za harusi, Harusi, Watumbatu, Harusi za watumbatu