Uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma: Mifano kutoka shule za msingi Tanzania

dc.creatorStephano, Rehema
dc.date2019-09-03T10:00:08Z
dc.date2019-09-03T10:00:08Z
dc.date2015
dc.date.accessioned2022-10-20T13:54:03Z
dc.date.available2022-10-20T13:54:03Z
dc.descriptionTasnifu ya uzamivu
dc.descriptionUtafiti huu umechunguza uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania zinazotumia mchepuo wa Kiswahili, hasa kwa kujikita katika mtaala wa Kiswahili. Malengo mahususi yaliyoshughulikiwa na utafiti huu ni matatu. Malengo hayo ni kuchambua viakifishi vinavyotumiwa katika uandishi wa kitaaluma wa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania, kuchunguza makosa ya uakifishaji yanavyojitokeza katika kazi za wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania na kubainisha sababu mbalimbali za makosa ya uakifishaji kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania. Utafiti huu umetumia mbinu mseto katika kukusanya data. Vilevile, umetumia mkabala wa kiidadi na wa kitaamuli kuwasilisha na kujadili data. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba wanafunzi wa Shule za Msingi wanafundishwa na wanatumia viakifishi vichache. Viakifishi hivyo ni nukta, kiulizo, mkato na mshangao, huku vingine vikitumika mara chache. Pia, matokeo ya utafiti yameonesha kuwa wanafunzi hawawezi kuakifisha kazi zao kwa usahihi kwa sababu hawafundishwi uakifishaji kwa kina, marefu na mapana. Kwa hali hiyo, wanafunzi hao huandika sentensi bebanifu, sentensi tata na vipande sentensi. Kwa hiyo, utafiti huu unapendekeza uakifishaji kufundishwa kama mada inayojitegemea katika viwango vyote vya elimu, Shule za Msingi, Sekondari hadi Vyuo Vikuu, ili wanafunzi waweze kuzielewa sheria na kanuni za uakifishaji na hivyo kuboresha maandiko yao ya kitaaluma.
dc.identifierStephano, R. (2015). Uzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma: Mifano kutoka shule za msingi Tanzania (Tasnifu ya uzamivu). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.
dc.identifierhttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1543
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/1543
dc.publisherThe University of Dodoma
dc.subjectUandishi wa kitaaluma
dc.subjectViakifishi
dc.subjectShule za msingi
dc.subjectTanzania
dc.subjectUzingatizi
dc.subjectMakosa ya uakifishaji
dc.subjectUchambuzi wa viakifishi
dc.titleUzingatizi wa viakifishi katika uandishi wa kitaaluma: Mifano kutoka shule za msingi Tanzania
dc.typeThesis

Files

Collections