Usawiri wa mwanamke katika muziki wa nyimbo za dansi: mifano kutoka katika nyimbo za Mbaraka Mwinshehe

dc.creatorSelemani, Suzana
dc.date2019-08-20T08:48:42Z
dc.date2019-08-20T08:48:42Z
dc.date2015
dc.date.accessioned2022-10-20T13:54:36Z
dc.date.available2022-10-20T13:54:36Z
dc.descriptionTasnifu (Shahada ya Uzamili ya Sayansi Jamii katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.descriptionUtafiti huu ulijadili kuhusu Taswira ya mwanamke katika Muziki wa Nyimbo za Dansi teule za Mbaraka Mwinshehe. Tatizo lililojenga utafiti huu ni kutokana na hali ya kila siku iliyopo kwa wasanii wa muziki wa nyimbo za dansi, wakiwemo wanaume, kumkweza mwanaume kinafasi na kimajukumu na kumtweza mwanamke. Utafiti ulitumia mbinu ya maktabani kwa kuchunguza kazi mbalimbali zilizoandikwa kuhusu usawiri wa mwanamke na mgawanyo wa majukumu kijinsia. Pia, nyimbo teule za Mbaraka Mwinshehe zimesikilizwa kwa makini ili kuweza kujua ni jinsi gani mwanamke amechorwa. Pia, mahojiano yalifanyika ili kuweza kupata na kuelewa kwa undani mada ya utafiti. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya Ufeministi, hususani wa Kiafrika, ambao una mawazo yanayozungumzia harakati za kumkomboa mwanamke katika jamii inayomdharau na kumkandamiza. Utafiti umebaini kuwa kuna tofauti kubwa za kimajukumu kati ya mwanamume na mwanamke katika jamii. Kwa asilimia kubwa, mwanamke amechorwa kwa upande hasi, yaani mnyonge, tegemezi na kiumbe duni. Hali imefanya mwanamke azidi kudharaulika, kutothaminiwa na kukejeliwa. Kwa kiasi kidogo, amechorwa ni mtu muhimu katika familia, hususani katika suala la kumstarehesha mwanaume awapo na shida. Vile vile, utafiti umebaini kuwa kuna athari kubwa kwa jamii zinazosababishwa na usawiri wa mwanamke katika nyimbo za dansi. Athari mojawapo ni kwa wasomaji kuiga matendo mabaya ambacho ni chanzo cha mwanamke kuendelea kudharaulika na kutothaminika katika jamii. Athari nyingine ni kuiga yale mema yanayompa hamasa mwanamke kuendelea kujituma katika majukumu mbalimbali. Hitimisho la Tasnifu hii ni kwamba mwanamke amekuwa ni mtu wa kutwezwa wakati huo mwanaume anakwezwa. Yote hayo yanasababishwa na mila na tamaduni mbovu zilizopo katika jamii ambazo zinamchukulia mwanamke kama kiumbe kisichoweza wakati wote na kuwa kinahitaji msaada kila wakati. Hata hivyo, utafiti umebaini kuwa ukweli hauko hivyo, mwanamke anaweza kuleta maendeleo bila utegemezi.
dc.identifierSelemani, S. (2015). Usawiri wa mwanamke katika muziki wa nyimbo za dansi: mifano kutoka katika nyimbo za Mbaraka Mwinshehe. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifierhttp://hdl.handle.net/20.500.12661/990
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/990
dc.languageKisw
dc.publisherChuo Kikuu cha Dodoma
dc.subjectUsawiri
dc.subjectMwanamke
dc.subjectUsawiri wa mwanamke
dc.subjectMuziki
dc.subjectNyimbo
dc.subjectDansi
dc.subjectNyimbo za dansi
dc.subjectMbaraka Mwinshehe
dc.titleUsawiri wa mwanamke katika muziki wa nyimbo za dansi: mifano kutoka katika nyimbo za Mbaraka Mwinshehe
dc.typeDissertation

Files