Nafasi ya utani wa sokoni na dikoni kwa jamii ya Wazanzibari

No Thumbnail Available

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Description

Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
Utafiti huu uliangalia nafasi ya utani wa sokoni na dikoni kwa jamii ya Wazanzibari. Utafiti uliongozwa na malengo matatu ambayo yalisaidia kubainisha nafasi ya utani wa sokoni na dikoni kwa jamii ya Wazanzibari. Tafiti zinazohusu utani nyingi zamezungumzia juu ya utani wa makabila na kwenye matukio ya sherehe na misiba na kutoa nafasi kwa mtafiti kuuchunguza utani katika muktadha huu. Utafiti ulifanyika uwandani na maktabani, na kutumia mbinu ya usaili, udodosaji, na ushuhudiaji katika kukusanya data. Maeneo yaliyotumika katika ukusanyaji wa data ni soko la Mwanakwerekwe na diko la Maruhubi katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Data zilichambuliwa kwa kuongozwa na nadharia ya utambulisho wa kijamii ambayo misingi yake mikuu ni utambulisho wa kijamii, ulinganishi katika jamii pamoja na matabaka na mgawanyiko katika jamii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa utani wa sokoni na dikoni una nafasi kubwa kwa jamii kwa jamii ya Wazanzibari. Utani huzuka kutokana na sababu tofauti za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni. Na hujengeka zaidi kwa maneno yenye ubeuzi dhihaka na utwezaji; na mara chache hutambwa kimatendo. Aidha, utani umekuwa ni chachu ya kuleta maelewano na udugu kwa watumiaji wa soko na diko na kupeleka mbele gurudumu la maisha yao. Zaidi, utafiti umegundua kuwa jadi hii bado wanajamii wanaikubali na ipo haja ya kuiendeleza kwani utani kwa wao ni kitambulisho cha utamaduni wao. Nadharia ya Utambulisho wa Jamii iliyotumika ilisaidia kufafanua jinsi utani unavyowatambulisha watu kwa hadhi zao, kazi zao na kutofautiana baina yao katika muktadha wa sokoni na dikoni.

Keywords

Utani, Sokoni, Utani wa sokoni, Dikoni, Utani wa dikoni, Wazanzibari

Citation