Dhima ya nyimbo za bongo fleva zihusuzo rushwa katika kuleta mabadiliko kwa jamii
No Thumbnail Available
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dodoma
Abstract
Description
Tasnifu (shahada ya Uzamili ya Sayansi Jamii katika Fasihi ya Kiswahili)
Utafiti huu ulilenga katika kuchunguza Dhima ya Nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo Rushwa katika kuleta Mabadiliko kwa Jamii. Bongo Fleva ni nyimbo za kizazi kipya nchini Tanzania. Nyimbo hizi huwa na dhamira mbalimbali ambazo hulenga kuelimisha na kuburudisha jamii inayokusudiwa na msanii. Njia ya nyimbo huwa bora zaidi kwani huwafikia sehemu kubwa ya jamii. Kutokana na umuhimu wa nyimbo jamii hupata mwitikio na kuifanya jamii kupata mabadiliko na kuifanya jamii mpya yenye maadili mema. Nyimbo mara nyingi husadifu mazingira ya jamii anapoimbia msanii na zinalenga vyema katika kutambulisha utamaduni wetu kwa kuyaweka mambo yetu. Utafiti huu uliongozwa na malengo ya aina mbili ambayo ni lengo la jumla la utafiti ambalo lilikuwa kuchunguza dhima ya nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa kwa mabadiliko ya jamii. Pia malengo mahususi matatu, Kwanza kukusanya nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa zinazoimbwa na wasanii mbalimbali katika Jamii, Pili kuchunguza na kuainisha dhima zinazopatikana katika nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa, na Tatu kuchunguza mwitikio wa jamii kuhusiana na nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa. Utafiti huu katika nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa tulizozisikiliza na kuzitumia kama kifani chetu tulibaini dhima mbalimbali kama vile kuelimisha, kuarifu, kukemea, kuadili, kuonya, ukombozi, kudhihaki uoga, kutia hamasa, kupitisha amali za jamii na kutumika kama rekodi ya matukio muhimu katika jamii. Utafiti huu ulifanyika maktabani na uwandani, maeneo mbalimbali ya halmashauri ya jiji la Mbeya yalitumika katika kukusanya data. Nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa zilikusanywa na kuwekwa katika maandishi, kisha kuchambuliwa na kupata dhima zinazopatikana katika nyimbo kwa mabadiliko ya jamii. Mwitikio wa jamii kuhusiana na nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa na mwisho mabadiliko yaliyopatikana kutokana na nyimbo. Uchambuzi wa data umefanywa kwa kutumia mkabala wa U-marx, Matokeo yanaonesha U-marx unajikita katika kuleta mabadiliko kwa kujua historia ya jambo na kuelewa tatizo kisha kuliunda upya kwa namna bora zaidi tofauti na awali. Pia nyimbo za Bongo Fleva zihusuzo rushwa zimewekwa katika maandishi.

Keywords
Nyimbo, Nyimbo za bongo Fleva, Rushwa, Kizazi kipya, Dhima ya fasihi, Mbeya, Tanzania