Ulinganishi wa kidhamira wa nyimbo za bongo fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku
dc.creator | Mtey, Felister Julius | |
dc.date | 2019-08-21T06:56:13Z | |
dc.date | 2019-08-21T06:56:13Z | |
dc.date | 2015 | |
dc.date.accessioned | 2022-10-20T13:54:34Z | |
dc.date.available | 2022-10-20T13:54:34Z | |
dc.description | Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili) | |
dc.description | Utafiti huu umechunguza suala la Ulinganishi wa Kidhamira wa Nyimbo za Bongo Fleva na Hadithi Fupi za Magazeti ya Udaku, kwa kutumia nyimbo za Bongo Fleva na hadithi fupi zilizomo ndani ya Magazeti ya Udaku. Mtafiti alipata wazo la kufanya utafiti huu kutokana na watafiti wengi kujikita katika lugha, matatizo yanayowakumba wanamuziki, na katika hadithi; kuchunguza athari za dhamira, hadithi za makabila, na hadithi fupi za Kiswahili. Lakini hakuna aliyelinganisha dhamira za muziki na hadithi. Kipengele cha ulinganishaji wa dhamira hakikupewa kipaumbele kutokana na kujikita zaidi katika kuchunguza vitu viwili kwa wakati mmoja. Mtafiti ameongozwa na nadharia ya Upokezi/mwitikio wa msomaji katika kuyafikia malengo yake. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kulinganisha dhamira za nyimbo za Bongo Fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku, ili kuona kama dhamira hizo zinafanana au kutofautiana katika jamii. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kwamba dhamira zilizopo ndani ya Muziki wa Bongo Fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku zinafanana, zinafanya kazi sawa na zina lengo moja katika jamii. Vile vile utafiti huu umeweza kuonyesha wazi, kuwa muziki wa Bongo Fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku vina mchango mkubwa katika jamii, kwani vinaelimisha, vinaburudisha, vinakosoa na kutoa muongozo katika jamii. Hivyo, watu wasivipuuze na kuona ni vitu visivyofaa na visivyokuwa na thamani katika jamii, au kuona ni vya kihuni na vinawahusu vijana tu. Bali watunzi na waandishi wazingatie zaidi tamaduni za Kiafrika, katika kuimba na kuandika kazi zao, pia katika uchapishaji wa magazeti hayo ya udaku na uvaaji wa wanamuziki vijana. | |
dc.identifier | Mtey, F. J. (2015). Ulinganishi wa kidhamira wa nyimbo za bongo fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku.Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma | |
dc.identifier | http://hdl.handle.net/20.500.12661/1035 | |
dc.identifier.uri | http://hdl.handle.net/20.500.12661/1035 | |
dc.language | Kisw | |
dc.publisher | Chuo Kikuu cha Dodoma | |
dc.subject | Dhamira | |
dc.subject | Nyimbo | |
dc.subject | Nyimbo za bongo Fleva | |
dc.subject | Hadithi | |
dc.subject | Hadithi fupi | |
dc.subject | Magazeti | |
dc.subject | Magazeti ya udaku | |
dc.subject | Bongo Fleva | |
dc.title | Ulinganishi wa kidhamira wa nyimbo za bongo fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku | |
dc.type | Dissertation |