Ukiukwaji wa nadharia tumizi ya uakifishaji katika kazi za kitaaluma za wanafunzi wa shule za msingi Tanzania

dc.creatorStephano, Rehema
dc.date2021-05-28T07:20:27Z
dc.date2021-05-28T07:20:27Z
dc.date2020
dc.date.accessioned2022-10-20T13:53:50Z
dc.date.available2022-10-20T13:53:50Z
dc.descriptionIkisiri. Makala kamili inapatikana https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/2462
dc.descriptionMakala haya ni zao la tasnifu ya Stephano (2015) yenye mada ya “Uzingatizi wa Viakifishi katika Uandishi wa Kitaaluma: Mifano kutoka Shule za Msingi Tanzania.” Makala inabainisha misingi mikuu ya Nadharia Tumizi ya Uakifishaji na kuonesha ukiukwaji wake katika nyaraka zinazotumika kufundishia na kujifunzia Kiswahili katika shule za msingi. Data za utafiti huu zimetokana na mapitio ya nyaraka za kufundishia na kujifunzia Kiswahili. Nyaraka hizo ni vitini vya masomo ya wanafunzi wa Darasa la VI na VII, na vitabu vya kiada na viongozi vya walimu Darasa I - VII. Matokeo ya uchunguzi wetu yanaonesha kuwa Nadharia Tumizi ya Uakifishaji haizingatiwi kwa uhakika, hasa katika uandishi wa insha. Ni viakifishi vichache tu, nukta, kiulizo, mshangao (viakifishi vya Safu 1) na mkato (kiakifishi cha Safu 4) ikilinganishwa na idadi inayopendekezwa na nadharia (ambavyo ni viakifishi kumi na vinne), ndivyo vinavyotumika. Zaidi, matokeo yanaonesha kuwa, pamoja na kutumika, viakifishi hivyo havitumiki kwa usahihi. Kwa hiyo, makosa ya kuandika sentensi bebanifu, sentensi tata na vipande sentensi hutokea. Makala yanapendekeza Nadharia Tumizi ya Uakifishaji kuzingatiwa wakati wa kuandika ili kuandika matini zinazoeleweka kwa wasomaji.
dc.identifierStephano, R. (2020). Ukiukwaji wa nadharia tumizi ya uakifishaji katika kazi za kitaaluma za wanafunzi wa shule za msingi Tanzania.Jarida la Taasisi la Taaluma za Kiswahili, Juz. 153(37)
dc.identifierURL: https://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/2462
dc.identifierhttp://hdl.handle.net/20.500.12661/3257
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.12661/3257
dc.languageKisw
dc.publisherTaasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
dc.subjectNadharia uakifishaji
dc.subjectWanafunzi shule msingi
dc.subjectTumizi uakifishaji taaluma
dc.subjectKiswahili
dc.subjectNadharia tumizi uakifishaji matini
dc.subjectShule msingi
dc.subjectTanzania
dc.titleUkiukwaji wa nadharia tumizi ya uakifishaji katika kazi za kitaaluma za wanafunzi wa shule za msingi Tanzania
dc.typeArticle

Files