Lugha ya Mazungumzo na ya Maandishi ni njia tofauti za mawasiliano zinazotumiwa na wanadamu. Hata hivyo baadhi ya sifa za lugha ya mazungumzo hujitokeza katika lugha ya maandishi na za lugha ya maandishi hujitokeza katika lugha ya mazungumzo. Mwingiliano huo husababisha uchanganyaji wa miundo ya njia hizi mbili za mawasiliano kwa baadhi ya waandishi. Lengo la makala haya ni: Mosi, kubainisha sifa za lugha ya mazungumzo na ya maandishi hasa katika kipengele cha muundo. Pili, kuonesha mwingiliano wa sifa hizo na sababu zake. Tatu, kutathmini athari za mwingiliano huo katika uandishi wa kitaaluma wa insha za wanafunzi. Inatarajiwa kuwa makala haya yatasaidia kupanua uelewa wa wanafunzi na waandishi kwa jumla kuhusu taratibu za uandishi, hasa wa kitaaluma.
Binafsi