Uambatizi ni mchakato mmojawapo wa kimofolojia unaohusu uundaji wa maneno. Mchakato huu huhusisha kategoria mbalimbali za maneno, kama vile nomino, vitenzi, vivumishi, vimilikishi, na vioneshi (Kiango, 2000). Vipengele mbalimbali ndani ya kategoria hizo huweza kutofautiana kutoka lugha moja hadi nyingine kutegemeana na sarufi ya lugha husika. Lengo la makala hii ni kuchunguza na kudhihirisha jinsi baadhi ya vipengele vya uambatizi wa vitenzi vinavyojitokeza katika Kishambala. Uchunguzi huu mdogo ni sehemu ya uchunguzi mpana unaolenga kuchambua sarufi ya Kishambala, kazi iliyoanzishwa na wataalamu kadhaa, mmojawapo akiwa marehemu Prof. Besha (1985)
Self