COSTECH Integrated Repository

Mabadiliko ya kasida: dhima na uwasilishaji

Show simple item record

dc.creator Issa, Mwanamosi Dude
dc.date 2019-08-20T10:52:58Z
dc.date 2019-08-20T10:52:58Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:35Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:35Z
dc.identifier Issa, M. D. (2015). Mabadiliko ya kasida: dhima na uwasilishaji. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/1008
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/1008
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Utafiti huu ulilenga kuchunguza mabadiliko ya kasida katika dhima na uwasilishaji wake Zanzibar ambao ulifanyika katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza mabadiliko ya kasida katika jamii ya Zanzibar katika dhima na uwasilishaji wake. Malengo mahsusi yalikuwa ni kutambulisha mabadiliko ya dhima yaliyojitokeza katika kasida za Kiswahili zinazotumiwa na jamii ya watu wa Zanzibar, kubainisha mabadiliko katika uwasilishaji wa kasida za Kiswahili zinazotumiwa na jamii ya Zanzibar pamoja na kuona athari za mabadiliko hayo. Mtafiti alitumia utaratibu wa uwandani na wa maktabani ambao ulitumia njia ya upekuzi wa marejeleo, uchunguzi shirikishi pamoja na usaili. Jumla ya kasida ishirini zilizilifanyiwa utafiti wa kina pamja na watafitiwa hamsini wakiwemo wazazi, walimu pamoja na wanafunzi wa madrasa. Nadharia ya Ubadilikaji Taratibu ndiyo iliyomuongoza mtafiti katika uchanganuzi wa data hizo zilizoteuliwa. Utafiti umeonesha kuwa yapo mabadiliko mbali mbali ya kasida katika uwasilishaji wa kasida pamoja na maudhui ya kasida katika jamii ya Wazanzibari na kwamba kasida husomwa kulingana na muktadha au matukio mbali mbali yanayojitokeza katika jamii husika. Pia utafiti uligundua kwamba kasida za Kiswahili zina nafasi nzuri katika kujenga maadili ya jamii husika kwani zimejikita karibu katika kila nyanja ya maisha ya Mzanzibari. Utafiti huu umeshauri jamii pamoja na wadau mbali mbali kuendeleza na kulinda hadhi ya kasida ili kuweza kutunza maadili ya jamii ya watu wa Zanzibar.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Kasida
dc.subject Mabadiliko ya kasida
dc.subject Dhima
dc.subject Dhima ya kasida
dc.subject Uwasilishaji
dc.subject Uwasilishaji wa kasida
dc.subject Zanzibar
dc.subject Mjini Magharibi Unguja
dc.title Mabadiliko ya kasida: dhima na uwasilishaji
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
MWANAMOSI DUDE ISSA.pdf 1.769Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account