COSTECH Integrated Repository

Athari ya matumizi ya mafumbo na tamathali za semi katika nyimbo za ngoma ya puuo kwa Wazanzibari

Show simple item record

dc.creator Mberwa, Abdi Ramadhan
dc.date 2019-01-18T08:53:19Z
dc.date 2019-01-18T08:53:19Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:32Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:32Z
dc.identifier Mberwa, A. R. (2015). Athari ya matumizi ya mafumbo na tamathali za semi katika nyimbo za ngoma ya puuo kwa Wazanzibari. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/542
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/542
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili ya Sayansi za Jamii katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Kazi hii imedhamiria kufafanua athariya matumizi ya mafumbo na tamathali za semi zinazojitokeza katika nyimbo zinazoimbwa katika muktadha wa uganga wa puuo. Lugha inayotumika katika nyimbo hizo huwa teule na yenye ukwasi mkubwa katika utumiaji wa mafumbo na tamathali, kama vile ishara, methali, taswira, taashira, tashbiha na tashhisi. Aidha, utafiti huu umelenga kubainisha athari zinazojitokeza kutokana na matumizi ya mafumbo na tamathali za semi kwa jamii ya Wazanzibari. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Semiotiki kwa kuzingatia mihimili yake katika kutafsiri ishara za kimafumbo na kitamathali zilizojitokeza katika nyimbo za ngoma ya puuo.Puuo ni aina ya ngoma ya uganga wa jadi ambayo hufanyika kwa baadhi ya jamii ya Wazanzibari ikiwa kama ni sehemu ya tiba kwa baadhi ya maradhi. Utamaduni huo upo na unaendelea kukua. Utafitiumegundua kuwepo kwa ukizani wa kimaana, ujumbe na dhima katika nyimbo za puuo kwa kupitia mitazamo na kauli za wasailiwa. Kwa hivyo, utafiti huu umetoa mchango katika kipengele cha fasihi simulizi kwani, tafiti zinazoelezea nyimbo za uganga wa jadi ni kidogo katika visiwa vya Zanzibar. Data zimekusanywa uwandani katika kijiji cha Umbuji na Dunga, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Udurusu wa maandiko katika maktaba umesaidia kupata maelezo ya jinsi ya kutumia mafumbo na tamathali katika muktadha wake. Aidha, mbinu ya usaili, ushuhudiaji na udurusu wa matini umetumika katika kukusanyia data. Data zilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti pamoja misingi ya Nadharia ya Semiotiki. Mwisho, matokeo ya utafiti huu yamewasilishwa kwa njia ya maelezo.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Mafumbo
dc.subject Tamathali za semi
dc.subject Nyimbo
dc.subject Ngoma
dc.subject Ngoma ya puuo
dc.subject Wazanzibari
dc.subject Uganga
dc.subject Lugha
dc.subject Nadharia ya Semiotiki
dc.subject Tamathali
dc.subject Semiotiki
dc.title Athari ya matumizi ya mafumbo na tamathali za semi katika nyimbo za ngoma ya puuo kwa Wazanzibari
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
ABDI RAMADHAN MBERWA.pdf 980.4Kb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account