Full text can be accessed at
http://www.ajol.info/index.php/ksh/article/view/79894
Makala haya yanajadili suala la lugha na uhusiano wake na watawala na wanasiasa. Ingawa yanatoa mifano ya nafasi ya lugha katika kuwainua wanasiasa na dhima yake katika ulinzi na usalama, mjadala unalenga kuiangalia lugha ya Kiswahili na nafasi yake katika uwezekano wa kuwa lugha inayotumika Afrika yote. Lugha ya Kiswahili inalinganishwa na silaha ambayo haina budi kutumiwa na nchi za Kiafrika katika kujenga na kuulinda Uafrika. Swali kubwa ni: je, ni kwa nini wanasiasa huitumia tu lugha ili kujiinua na kisha kuiacha kando ikiisha kuwatimizia haja zao? Suala hili ni changamoto kubwa kwa wanasiasa ambao huwa watawala wanaozingatia masilahi yao binafsi. Haya ni makala ya kiuchambuzi ambayo yanalenga kuibua mjadala kuhusu hatua ambazo hazinabudi kuchukuliwa ili kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya Waafrika.