COSTECH Integrated Repository

Taswira katika Ngano za Kiswahili kutoka Wilaya ya Kusini Unguja-Zanzibar

Show simple item record

dc.creator Mwinyi, Hassina Yussuf
dc.date 2019-08-20T11:16:48Z
dc.date 2019-08-20T11:16:48Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:34Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:34Z
dc.identifier Mwinyi, H. Y. (2015). Taswira katika Ngano za Kiswahili kutoka Wilaya ya Kusini Unguja-Zanzibar. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/1013
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/1013
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Utafiti huu ulihusu taswira zinazojitokeza katika ngano za Kiswahili. Utafiti huu ulifanyika katika vijiji vya Wilaya ya Kusini, Unguja. Lengo kuu la utafiti huu nikuchambua taswira zinazojitokeza katika ngano za Kiswahili. Malengo mahsusi yalikuwa ni kubainisha na kuchambua taswira zinazojitokeza katika ngano za Kiswahili, kuchunguza sababu zinazoibua mitindo ya lugha katika taswira za ngano na kuchambua uwiano wa kitaswira na kidhamira kati ya ngano na jamii. Jumla ya ngano kumi na nne zilifanyiwa uchambuzi wa kina pamoja na watafitiwa ishirini na nane wakiwemo wazee ambao wana tajriba kuhusu ngano. Kwa upande wa walimu na wanafunzi walitafitwa kwa sababu wao ndio wana uelewa mkubwa kuhusu dhana ya taswira. Katika mchakato wa ukusanyaji data, mtafiti alitumia utaratibu wa uwandani na wa kimaktaba ambao ulitumia njia ya upekuzi wa marejeleo, ushuhudiaji na usaili. Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji ilitumika wakati wa kuwasilisha na kufafanua data za utafiti huu. Uchambuzi wa taswira za ngano za Kiswahili uliofanywa katika sura ya nne umetoa matokeo mengi, matokeo hayo ni kama; utafiti ulibaini kuwa lugha inayotumika katika ngano ni lugha ya kitaswira, haswa matumizi ya taswira za hisi, taswira za kuonekana na taswira za mawazo. Pia utafiti uligundua kwamba taswira hizo zinatoa uhuru wa kuyaeleza mambo mazito yanayoizunguka jamii ya watu wa Wilaya ya Kusini. Halikadhalika, utafiti uliona kuwa zaidi ya taswira moja inaweza ikatumika katika ngano moja. Utafiti huu umetoa maoni kwa Serikali ya Mapinduzi ichukuwe juhudi za makusudi kuingiza utanzu wa ngano katika mtaala wa elimu ili ziweze kufundishwa kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vikuu. Wazazi nao wanajukumu la kupata muda wa kuwasimulia ngano watoto wao ili kujenga maadili mema na iwe hazina na urithi bora.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Taswira
dc.subject Ngano
dc.subject Kiswahili
dc.subject Ngano za Kiswahili
dc.subject Kusini Unguja
dc.subject Zanzibar
dc.title Taswira katika Ngano za Kiswahili kutoka Wilaya ya Kusini Unguja-Zanzibar
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
HASSINA YUSSUF MWINYI.pdf 916.9Kb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account