COSTECH Integrated Repository

Ulinganishi wa kidhamira wa nyimbo za bongo fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku

Show simple item record

dc.creator Mtey, Felister Julius
dc.date 2019-08-21T06:56:13Z
dc.date 2019-08-21T06:56:13Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:34Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:34Z
dc.identifier Mtey, F. J. (2015). Ulinganishi wa kidhamira wa nyimbo za bongo fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku.Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/1035
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/1035
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Utafiti huu umechunguza suala la Ulinganishi wa Kidhamira wa Nyimbo za Bongo Fleva na Hadithi Fupi za Magazeti ya Udaku, kwa kutumia nyimbo za Bongo Fleva na hadithi fupi zilizomo ndani ya Magazeti ya Udaku. Mtafiti alipata wazo la kufanya utafiti huu kutokana na watafiti wengi kujikita katika lugha, matatizo yanayowakumba wanamuziki, na katika hadithi; kuchunguza athari za dhamira, hadithi za makabila, na hadithi fupi za Kiswahili. Lakini hakuna aliyelinganisha dhamira za muziki na hadithi. Kipengele cha ulinganishaji wa dhamira hakikupewa kipaumbele kutokana na kujikita zaidi katika kuchunguza vitu viwili kwa wakati mmoja. Mtafiti ameongozwa na nadharia ya Upokezi/mwitikio wa msomaji katika kuyafikia malengo yake. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kulinganisha dhamira za nyimbo za Bongo Fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku, ili kuona kama dhamira hizo zinafanana au kutofautiana katika jamii. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kwamba dhamira zilizopo ndani ya Muziki wa Bongo Fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku zinafanana, zinafanya kazi sawa na zina lengo moja katika jamii. Vile vile utafiti huu umeweza kuonyesha wazi, kuwa muziki wa Bongo Fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku vina mchango mkubwa katika jamii, kwani vinaelimisha, vinaburudisha, vinakosoa na kutoa muongozo katika jamii. Hivyo, watu wasivipuuze na kuona ni vitu visivyofaa na visivyokuwa na thamani katika jamii, au kuona ni vya kihuni na vinawahusu vijana tu. Bali watunzi na waandishi wazingatie zaidi tamaduni za Kiafrika, katika kuimba na kuandika kazi zao, pia katika uchapishaji wa magazeti hayo ya udaku na uvaaji wa wanamuziki vijana.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Dhamira
dc.subject Nyimbo
dc.subject Nyimbo za bongo Fleva
dc.subject Hadithi
dc.subject Hadithi fupi
dc.subject Magazeti
dc.subject Magazeti ya udaku
dc.subject Bongo Fleva
dc.title Ulinganishi wa kidhamira wa nyimbo za bongo fleva na hadithi fupi za Magazeti ya Udaku
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
FELISTER JULIUS MTEY.pdf 783.2Kb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account