dc.creator |
Ussi, Ussi Juma |
|
dc.date |
2019-08-21T07:06:03Z |
|
dc.date |
2019-08-21T07:06:03Z |
|
dc.date |
2015 |
|
dc.date.accessioned |
2022-10-20T13:54:36Z |
|
dc.date.available |
2022-10-20T13:54:36Z |
|
dc.identifier |
Ussi, U. J. (2015).Suala la utendaji katika michezo ya jadi ya watoto: mfano kutoka Bumbwini- Zanzibar. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma |
|
dc.identifier |
http://hdl.handle.net/20.500.12661/1036 |
|
dc.identifier.uri |
http://hdl.handle.net/20.500.12661/1036 |
|
dc.description |
Tasnifu (Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Jamii Katika Fasihi) |
|
dc.description |
Utafiti huu umechunguza Utendaji Katika Michezo ya Jadi ya Watoto wa
Bumbwini, Zanzibar. Tasnifu hii ilizingatia dhana kwamba kuna mtazamo finyu
katika jamii kuhusiana na michezo ya watoto. Kuna wazo kuwa jamii imechukulia
michezo ya jadi ya watoto kuwa ni kuwaburudisha na kuwapa mazoezi ya kimwili
na kiakili tu. Kwa hivyo, utafiti huu umekusudia kubainisha dhima za utendaji
katika michezo ya jadi ya watoto ili kuondoa dhana potofu ya jamii kuhusiana na
michezo hiyo.
Katika kukamilisha lengo la utafiti, ukusanyaji wa data wa uwandani ulitumika ili
kuipata michezo kutoka katika sehemu husika inapochezwa. Usaili, hojaji na
ushuhudiaji ni mbinu ambazo zilitumika katika utafiti huu. Michezo mingi ilitafitiwa
ili kupata matokeo yaliyosahihi. Utafiti umeongozwa na nadharia ya Uamilifu
ambayo inahusiana na kipande kazi cha kazi ya fasihi jinsi kinavyoweza
kufanyakazi katika jamii. Nadharia ya uamilifu inazingatia matakwa ya jamii
kulingana na uhusiano uliopo katika jamii husika na jinsi fasihi inavyofanyakazi.
Nadharia hii imesaidia kubainisha michezo, miundo ya michezo na hatimae
kubainisha dhima mbalimbali zilizojitokeza katika utendaji wa michezo ya watoto.
Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa kuna dhima nyingi zinazotekelezwa
katika michezo ya jadi ya watoto. Dhima zimebainika kutokana na nadharia
iliyotumika ambayo imejikita katika kuiangalia jamii na matakwa yake katika
maisha ya kila siku. Utafiti umebaini kuwa michezo ya watoto inawakilisha matendo
ya kila siku ya wanajamii na ambayo yanasawiri majukumu ya watu katika jamii
husika. Kwa hivyo, utafiti umefuta dhana ya kuwa michezo ya watoto ni kupoteza
muda au kuwaburudisha watoto tu. |
|
dc.language |
Kisw |
|
dc.publisher |
Chuo Kikuu cha Dodoma |
|
dc.subject |
Michezo |
|
dc.subject |
Jadi |
|
dc.subject |
Watoto |
|
dc.subject |
Jadi ya watoto |
|
dc.subject |
Bumbwini |
|
dc.subject |
Zanzibar |
|
dc.title |
Suala la utendaji katika michezo ya jadi ya watoto: mfano kutoka Bumbwini- Zanzibar |
|
dc.type |
Dissertation |
|