COSTECH Integrated Repository

Ujumi katika hotuba teule za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Show simple item record

dc.creator Shilindi, Manfred Raphael
dc.date 2019-08-21T09:13:01Z
dc.date 2019-08-21T09:13:01Z
dc.date 2015
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:34Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:34Z
dc.identifier Shilindi, M. R. (2015). Ujumi katika hotuba teule za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/1045
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/1045
dc.description Tasnifu (Shahada ya Uzamili ya Fasihi ya Kiswahili)
dc.description Tasnifu hii ni matokeo ya utafiti uliojikita katika kufanya uchambuzi wa vipengele vya kiujumi katika Fasihi simulizi, hususani katika hotuba teule za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Madhumuni ya tasnifu hii ni kuweka wazi vipengele vya kiujumi vilivyomo katika hotuba hizo ili kuonesha uthibitisho kuwa taaluma ya ujumi inayo nafasi kubwa katika Fasihi simulizi. Pia tumefanya uchambuzi ili kuweza kuwianisha vipengele vya ujumi vinavyopatikana katika hotuba hizo na hali halisi ya maisha ya Watanzania, pamoja na kubainisha athari za kiujumi. Utafiti huu ulifanyika maktabani na uwandani ulitumia mbinu ya uchambuzi wa matini, pamoja na mahojiano. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa njia ya ufafanuzi na data tulizozipata ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Aidha, vielelezo vilitumika. Utafiti huu ulimakinikiwa na kuongozwa na mkabala wa Ki- Marx ambao ni mkabala unaotumia mbinu za kiupembuzi katika kuchanganua mambo ya kijamii na kiutamaduni. Kwa jumla, ili kumakinika vema katika masuala ya kiujumi, hatuna budi kuwa na utambuzi wa idili za jamii husika. Tasnifu hii ina jumla ya sura tano. Sura ya kwanza imeeleza usuli wa mada, tamko la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, na mawanda ya utafiti. Sura ya pili imeeleza mapitio ya maandiko yanayohusu ujumi na hotuba, pamoja na mapengo yaliyojitokeza. Sura ya tatu ya mchakato huu tumeeleza mbinu za utafiti, eneo la utafiti na vifaa vya utafiti, pamoja na mkabala wa utafiti. Njia zilizotumika katika kukusanya data ni mbinu ya uchambuzi wa matini, pamoja na mahojiano. Sura ya nne uwasilishaji na uchambuzi wa data. Uchambuzi kuhusiana na masuala ya kiujumi katika hotuba hizo. Sura ya tano ambayo ndiyo sura ya mwisho kwa mujibu wa tasnifu hii, inahusu hitimisho na mapendekezo.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Ujumi
dc.subject Fasihi
dc.subject Fasihi simulizi
dc.subject Hotuba
dc.subject Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
dc.subject Hotuba za Mwalimu
dc.title Ujumi katika hotuba teule za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
MANFRED RAPHAEL SHILINDI.pdf 1.279Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account