COSTECH Integrated Repository

Suala la ufungwa katika ushairi wa kiswahili: mifano kutoka diwani za sauti ya dhiki na chembe cha moyo

Show simple item record

dc.creator Hamad, Maryam Ali
dc.date 2018-10-09T08:07:00Z
dc.date 2018-10-09T08:07:00Z
dc.date 2017
dc.date.accessioned 2022-10-20T13:54:32Z
dc.date.available 2022-10-20T13:54:32Z
dc.identifier Hamad, M. A. (2017). Suala la Ufungwa katika ushairi wa kiswahili: mifano kutoka diwani za sauti ya dhiki na chembe cha moyo. Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.identifier http://hdl.handle.net/20.500.12661/454
dc.identifier.uri http://hdl.handle.net/20.500.12661/454
dc.description Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili
dc.description Tasnifu hii inajadili suala la ufungwa katika diwani za Sauti ya Dhiki (1973) na Chembe cha Moyo (1988). Tatizo lililomsukuma mtafiti kufanya utafiti huu ni kwa kuwa tafiti katika uga huu wa ufungwa bado ni finyu. Kwa kutumia nadharia ya uhemenitiki na nadharia ya Ki-Marx mtafiti alichunguza suala la ufungwa katika ushairi wa Kiswahili kwa kutumia diwani teule. Data zilikusanywa maktabani na uwandani maeneo ya Zanzibar, Kenya, Dar es Salaam na Dodoma. Mbinu zilizotumika katika utafiti huu ni udurusu wa maktabani, njia ya udodosaji na njia ya mahojiano. Data zilichanganuliwa kwa kuzingatia njia ya maelezo ya utafiti pamoja na misingi ya nadharia za Uhemenitiki na Ki-Marx. Utafiti umegundua namna ufungwa ulivyokabiliwa na vikwazo vikubwa katika jamii inayohusiana na wafungwa. Kwa hivyo, utafiti umetoa mchango mkubwa kuhusiana na suala la ufungwa katika kipengele cha fasihi andishi ya Kiswahili kwa upande wa ushairi. Mchango mpya ulioibuliwa kutokana na utafiti ni huu ufuatao: Utafiti umegundua matatizo yanayowapata wafungwa wa aina yoyote katika jamii, kwa mfano, ufungwa wa gerezani, mfungwa anapowekwa gerezani huteswa na hukatiwa matumaini yake yote katika mustakbali wa maisha yake. Pia, kumpotezea malengo kwa watu waliomzunguka akiwa kama ni muhimili mkuu wa jamii hiyo ikiwemo familia. Tatizo hili linaweza kurekebishika. Wafungwa badala kuadhibiwa vikali magerezani wakatumiwa kama rasilimali watu kwa kutumia ujuzi walionao kunufaisha jamii na taifa kwa jumla. Aidha, utafiti umeonesha namna ambavyo nadharia za Uhemenitiki na Ki-Marx kwa kutumia misingi yake ilivyokuwa faafu kwa utafiti huu.
dc.language Kisw
dc.publisher Chuo Kikuu cha Dodoma
dc.subject Sauti ya dhiki
dc.subject Chembe cha moyo
dc.subject Ufungwa
dc.subject Ushairi
dc.subject Fasihi
dc.subject Nadharia ya uhemenitiki
dc.subject Nadharia ya Ki-Marx
dc.subject Fasihi andishi
dc.subject Mafunzo
dc.subject Gerezani
dc.subject Kiswahili
dc.subject Familia
dc.subject Nadharia
dc.title Suala la ufungwa katika ushairi wa kiswahili: mifano kutoka diwani za sauti ya dhiki na chembe cha moyo
dc.type Dissertation


Files in this item

Files Size Format View
MARYAM HAMAD- RIPOTI.pdf 1.732Mb application/pdf View/Open

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search COSTECH


Advanced Search

Browse

My Account